Pata taarifa kuu
UKRAINE-URUSI

Madaraja yote yanayoendelekea mjini Severodonetsk yavunjwa

Nchini Ukraine, madaraja yote yanayounganisha mji wa Mashariki wa Severodonetsk yameharibiwa wakati huu wanajeshi wa Urusi wanapoendelea kushambulia mji huo.

Mji wa  Sievierodonetsk,uliosalia mahame
Mji wa Sievierodonetsk,uliosalia mahame AP - Oleksandr Ratushniak
Matangazo ya kibiashara

Gavana wa jimbo la Luhansk, Serhiy Haidai anasema, kuharibiwa kwa madaraja hayo, kumesabababisha ugumu wa kuwahamisha raia, lakini pia kutoa misaada ya dharura kama chakula na dawa.

Kwa wiki kadhaa sasa wanajeshi wa Urusi wamekuwa wakipambana kuuteka mji huo wa Severodonetsk, ili kudhibiti jimbo lote la Luhansk.

Wapiganaji wanaounga mkono wanajeshi wa Urusi katika wanaodhibiti mji huo sasa wanawataka wanajeshi wa Ukraine wajisalimishe la sivyo wauwawe.

Wakati hayo yakijiri, rais wa Ukraine amewaambia wananchi wa taifa lake kuwa, pamoja na jeshi la nchi yake kuendelea kukabiliwa vikali na Urusi, hatimaye, watakomboa miji na majimbo yote ya taifa hilo.

Hata hivyo, amesema gharama ya kulikomboa jimbo la Donbas ni kubwa, wakati huu uongozi wa polisi ukisema, unachunguza vifo vya raia Elfu 12 katika vita vinavyoendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.