Pata taarifa kuu
RWANDA-UINGEREZA

Mwanamfalme Charles akerwa na mpango wa kuwasafirisha wahamiaji nchini Rwanda

Mwanamfalme wa Uingereza Charles ameelezea mpango wa serikali ya nchi hiyo, kuwapeleka wahamiaji haramu nchini Rwanda, kama hatua ya kushtua kwa mujibu wa Gazeti la The Times.

Mwanamfalme Charles  wa Uingereza
Mwanamfalme Charles wa Uingereza REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Ripoti kutoka Uingereza, zinasema Mwanamfalme Charles anasikitishwa na mpango wa serikali ya Uingereza wakati huu, inapopanga kuwapelekea wahamiaji wa Kwanza nchini Rwanda hivi karibuni.

Ametoa kauli hii wakati huu pia, anapotarajiwa jijini Kigali baadaye mwezi huu kumwakilisha mama yake, Malkia Elizabeth wa pili wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Madola.

Mpango huu wa serikali ya Uingereza pia imeendelea kupingwa na wanaharakati wa haki za binadamu wanapotarajiwa kwenda Mahakamani wiki ijayo.

Uingereza inasema tayari imeshawapa tarifa wahamiaji 130 kuwa watasafirishwa nchini Rwanda kuanzia wiki ijayo, baada ya London na Kigali kuingia kwenye maelewano ya mpango huo mwezi Aprili.

Rwanda inasema iko tayari kuwapokea wahamiaji hao na kuwasaidia kwa ajili yao wenyewe na nchi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.