Pata taarifa kuu
UKRAINE-URUSI

Zelenskyy aishtumu Urusi kusababisha mamilioni ya watu kukabiliwa na baa la njaa

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy anaonya kuwa mamilioni ya watu  duniani wataendelea kukabiliwa na baa la njaa iwapo, Urusi itaendelea kuzuia usafirishwaji wa vyakula kutoka katika maeneo wanayodhibiti.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy AP
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na hali hii, Zelensky sasa anataka Urusi kuondolewa kwenye Tume ya Umoja wa Mataifa ya Chakula la Kilimo, wakati huu Umoja wa Mataifa ukionya kuwa dunia ipo kwenye hatari ya kukabiliwa na baa la njaa.

Rais huyo wa Ukraine pia anasema hali inaendelea kuwa mbaya katika mji wa Severodonetsk, ambao kwa kiasi kikubwa unadhibitiwa na vikosi vya Urusi, wakati huu watu elfu 10 wakikwama katika mji huo, wakati huu Urus ikisema wapiganani wa Uingereza na Morocco waliokamatwa nchini Ukraine wamehukumiwa kunyongwa.

Aidha, Umoja wa Mataifa não unaonya kuwa, uwekezaji wa moja kwa moja, katika mataifa mbalimbali, unatarajiwa kushuka, kufuatia uhaba wa chakula, mafuta na fedha kufuatia mzozo huu.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema jaribio lolote la kuilazimisha Ukraine kupata amani na Urusi, halikubaliki kwa sababu Moscow ndio iliyoivalia Kiev.

Kauli hii inakuja, baada ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wiki iliyopita, kusema kuwa, mataifa ya Magharibi yanapaswa kutoa nafasi kwa Urusi, ili kuona iwapo kuna nafas ya kidiplomasia ili kumaliza vita kati yake na Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.