Pata taarifa kuu

Volodymyr Zelensky kuhuhutubia viongozi wa Ulaya

Rais wa Ukraine anatazamiwa kuzungumza mwanzoni mwa mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya leo Jumatatu, kwa njia ya video kutoka mjini Kyiv.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akitembelea eneo la Kharkiv kaskazini mashariki mwa Ukraine mnamo Mei 29, 2022.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akitembelea eneo la Kharkiv kaskazini mashariki mwa Ukraine mnamo Mei 29, 2022. via REUTERS - UKRAINIAN PRESIDENTIAL PRESS SER
Matangazo ya kibiashara

Vikwazo vipya dhidi ya Moscow vitakuwa kwenye ajenda ya mkutano huu wa nchi Ishirini na Saba za Umoja wa Ulaya. Mbali na vikwazo vya mafuta, kifurushi cha vikwazo kinalenga kuziondoa benki za Urusi kutoka kwa mfumo wa kimataifa wa kifedha wa Swift, msaada kwa Ukraine wa hadi euro bilioni tisa mnamo mwaka 2022.

Siku ya Jumapili wawakilishi wa nchi 27 za Umoja wa Ulaya walijadili pendekezo jipya ambalo litaondoa kwa muda bomba muhimu la mafuta kwa Hungary kutoka vikwazo vya EU juu ya mafuta ya Urusi, katika jaribio la kuondoa mkwamo wa kifurushi cha sita cha vikwazo dhidi ya Moscow. Vikwazo hivi vipya kwa sasa vimezuiwa na Hungary, nchi isiyo na bahari na inayotegemea mafuta yanayoletwa kutoka Urusi kupitia bomba la Druzhba, ambalo huipatia 65% ya matumizi yake.

Hotuba hii ya Rais Zelensky inajiri siku moja baada ya ziara yake ya iliyozungumzia zaidi katikavyombo vya habari siku ya Jumapili huko Kharkiv, mji wa pili wa Ukraine, kaskazini-mashariki mwa nchi. Tutatetea nchi yetu. Hawana nafasi,” Zelensky alisema siku ya Jumapili, akikutana na askari katika uwanja wa vita, na kuzuru majengo yaliyoharibiwa huko Kharkiv.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.