Pata taarifa kuu

Kremlin akanusha kuwa Vladimir Putin ni mgonjwa

Mkuu wa diplomasia ya Urusi, Sergey Lavrov, amesema mara kadhaa kwenye kituo cha televisheni cha Ufaransa TF1 kwamba "ukombozi" wa Donbass ulikuwa kipaumbele kabisa cha Moscow, Kremlin ikiwa imetambua uhuru wa "jamhuri za watu" za Luhansk na Donetsk mwishoni mwa mwezi wa Februari.  Pia alikanusha uvumi kuhusu afya ya Vladimir Putin.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya mkutano wake na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres huko Moscow, Urusi, Aprili 26, 2022.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya mkutano wake na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres huko Moscow, Urusi, Aprili 26, 2022. REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya Urusi na Ukraine vimekabiliana vikali mashariki mwa Ukraine katika wakati jeshi la Urusi linatanua hujuma zake kujaribu kulikamata jimbo la Donbas.

Kwenye eneo hilo vikosi vya Urusi viliushambulia kwa makombora mji wa kimkakati wa Sievierodonetsk vikinuwia kuuzingira bila mafanikio.

Meya wa mji huo amesema mapigano yamesababisha kukatika kwa huduma ya umeme na simu na kumelazimisha kituo cha msaada wa kiutu kufungwa kutokana na hatari iliyopo.

Naibu mkuu wa Shirika la Mkataba wa Atlantiki ya Kaskazini (NATO), Mircea Geoana, alisema Jumapili kwamba NATO haizingatii tena ahadi zake za zamani kwa Moscow kutopeleka vikosi vyake Ulaya Mashariki.

Katika hatua ya kuanzisha uhusiano kati ya NATO na Urusi, iliyotiwa saini miaka 25 iliyopita, Urusi "iliahidi kutoshambulia majirani zake, jambo ambalohaitekelezi, na kufanya mashauriano ya mara kwa mara na NATO, ambayo haifanyi," Mircea Geoana alisema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.