Pata taarifa kuu
UKRAINE-URUSI

Vita vyaendelea mashariki mwa Ukraine huku, takwimu za waliouawa zikiwekwa wazi

Nchini Ukraine, wakati huu wanajeshi wa Urusi wanapoendelea kushambulia eneo la Mashariki mwa nchi hiyo, wapiganaji wanaoiunga mkono Urusi wanadai kudhibiti kikamilifu mji wa Lyman, Kaskaizini mwa jimbo la Donbas, wakati huu Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa ikitoa takwimu za watu waliopoteza maisha katika mzozo wa Ukraine.

Shambulio katika jimbo la  Donbass,nchini Ukraine.
Shambulio katika jimbo la Donbass,nchini Ukraine. AFP - ARIS MESSINIS
Matangazo ya kibiashara

Kwa mjibu wa Umoja wa mataifa tangu vita kuanza nchini Ukraine mwezi Februari, zaidi ya raia 4,031 wameuawa miongoni mwao watoto 200, wengi wa raia hawa wakidaiwa kuuawa na vilipuzi  na kutumika kama ngao, aidha Urusi imekana kuwalenga raia katika vita hivyo vinavyoendelea. 

Hayo yakijiri,  shambulio la Urusi katika kituo cha kijeshi cha Ukraine, limesabisha vifo vya watu 10 ijumaa, na kuwajeruhiwa wengine 30 

Kwingineko msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov, ametuhumu Ukraine kwa kulemeza mazungumzo ya kutafuta amani, naye rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, amesema Ukraine inataka mazungumzo ya amani yatakayomhusisha rais Putin mwenyewe. 

Zelenskyy pia ameongeza kuwa uvamizi wa urusi katika eneo la Donbas litabisha eneo hilo kusalia mahame, na kwamba Mosco inapanga kuteketeza, miji ya Popasna, Lysychansk na Severodonetsk 

Aidha Urusi pia imewafukuza wafanyakzi watano wa Croatia kutoka nchini humo, ikiwa ni hatua ya kujibu Croatia iliowatimua wafanyakazi wa ubalozi wa Urusi, baada yake kuvamia Ukraine. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.