Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Vikosi vya Urusi vyshambulia zaidi ya miji 40 Donbass

Wakati wa Kongamano la Kiuchumi la Davos siku ya Jumatano, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kouleba aliishutumu NATO kwamba "haijafanya lolote" dhidi ya uvamizi wa nchi yake ulioanzishwa na Urusi, na alipendelea kupongeza "maamuzi ya mapinduzi" ya Umoja wa Ulaya. Pia aliomba silaha zaidi za kivita.

Gari iliyoteketea kwa moto kwenye barabara inayoelekea Popasna, Donbass, Aprili 2022.
Gari iliyoteketea kwa moto kwenye barabara inayoelekea Popasna, Donbass, Aprili 2022. AFP - RONALDO SCHEMIDT
Matangazo ya kibiashara

Mji wa viwanda wa Sievierodonetsk, magharibi mwa mkoa wa Luhansk, unakaribia kuzingirwa na jeshi la Urusi. Siku ya Jumatano, kwa mujibu wa jeshi la Ukraine, zaidi ya miji 40 ya Donbass ilishambuliwa kwa mabomu.

Urusi imetangaza kwamba itawaruhusu wakazi wa mikoa ya Zaporizhzhia na Kherson kuomba pasipoti ya Kirusi kupitia "utaratibu uliorahisishwa". Ukraine ilishutumu mara moja hatua inayoonyesha nia ya Moscow ya kukalia kwa urahisi maeneo haya.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imeahidi kufunguwa njia salama za kuzipisha meli za kigeni kuondoka kwenye bandari za Bahari Nyeusi. Mkuu wa Kituo cha Udhibiti wa Ulinzi wa Taifa cha Urusi, Mikhail Mizintsev, amesema njia nyengine itafunguliwa kuruhusu meli kuondoka mji wa bandari wa Mariupol kupitia Bahari ya Azov hadi Bahari Nyeusi.

Kwa mujibu wa Mizintsev, kuna meli 70 kutoka mataifa 16 ya kigeni kwenye bandari sita za Bahari Nyeusi, zikiwemo Odesa, Kherson na Mykolaiv.

Mapema jana, jeshi la Urusi lilisema bandari ya Mariupol imeanza tena kufanya shughuli zake baada ya miezi mitatu ya mapigano. Jeshi hilo, ambalo lina kituo chake ndani ya Bahari Nyeusi, limefanikiwa kuzuwia meli za kibiashara katika bandari za Ukraine kwa muda wote wa mapigano hadi sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.