Pata taarifa kuu

Olaf Scholz: Putin hatoshinda vita dhidi ya Ukraine

Moscow, ambayo imeanzisha mashambulizi makubwa dhidi ya Donbass kwa wiki kadhaa, inafanikiwa hatua kwa hatua kuliteka eneo hili la mashariki mwa Ukraine, hata kama jeshi la Ukraine linaweka upinzani mkali.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz katika Kongamano la Kiuchumi la Dunia huko Davos, Mei 26, 2022.
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz katika Kongamano la Kiuchumi la Dunia huko Davos, Mei 26, 2022. AP - Markus Schreiber
Matangazo ya kibiashara

Mji mkubwa wa Sievierodonetsk sasa unakaeibia kuzingirwa, kulingana na meya wa mji huo.

Wanajeshi wa Ukraine lakini pia vikosi vya Ulinzi  (FDT) wanaendelea kuhamasishwa.

Takriban kilomita mia moja kusini, katika mji wa Druzhkivka, FDT, inayoundwa na raia, hutoa misaada ya kibinadamu hasa. Aleksander alijiunga nao kutoka siku ya kwanza ya mzozo. Anatoa wito kwa nchi za Magharibi kuwapa msaada.

Donbass haitaanguka mradi tu tupo. Bila shaka tuna silaha, lakini hiyo haitoshi. Nchi za magharibi zinatutumia misaada, lakini haitoshi. Ikiwa tungekuwa na silaha na vifaa vya kutosha, hakuna mtu anayeweza kutuzuia kukaa Donbass. Jeshi la Urusi halina nguvu kama inavyofikiriwa. Lakini ni mara 20 zaidi kuliko jeshi letu, na silaha na rasilimali mara 20 zaidi. Nchi za Magharibi zikianza kuogopa kutusaidia, taratibu tutapoteza maana jeshi lao ni kubwa sana kwa majeshi yetu.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alisema siku ya Alhamisi kwamba ana iani kuwa Urusi haitashinda vita ilivovyoanzisha nchini Ukraine, akisema pia kwamba Rais Vladimir Putin hataruhusiwa "kuamuru masharti" ya amani.

"Putin hatoshinda vita vyake. Na nina uhakika hatashinda," kansela alisema wakati wa hotuba katika mkutano wa Jukwaa la Uchumi la Dunia huko Davos, Uswisi, akisema rais wa Urusi, ambaye alianzisha uvamizi wa Ukraine zaidi ya miezi mitatu iliyopita, "tayari amekosa malengo yake ya kimkakati".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.