Pata taarifa kuu

Vikosi vya Ukraine vyadai kuwa vimedhibiti tena enero la mpakani Kharkiv

Katika siku ya 82 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Jumatatu hii, Mei 16, Ukraine imedai kuwa udhibiti wa eneo la mpakani huko Kharkiv kutoka mikononi mwa Urusi.

Mwanajeshi wa Ukraine akipita mbele ya gari la kivita la Urusi lililoharibiwa karibu na Kutuzivka, kaskazini mwa Kharkiv, mashariki mwa Ukraine, Jumapili, Mei 15, 2022.
Mwanajeshi wa Ukraine akipita mbele ya gari la kivita la Urusi lililoharibiwa karibu na Kutuzivka, kaskazini mwa Kharkiv, mashariki mwa Ukraine, Jumapili, Mei 15, 2022. AP - Mstyslav Chernov
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya Ukraine vimewatimua wanajeshi wa Urusi na kurejesha udhibiti wa sehemu ya mpaka na Urusi katika eneo la Kharkiv (kaskazini mashariki), mamlaka ya Ukraine imetangaza Jumatatu.

Shinikizo la Urusi bado lina nguvu mashariki mwa Ukraine, hasa katika eneo la Donbass, ambapo Urusi ilikuwa imetangaza kwamba wataelekeza nguvu zao za kijeshi.

Hata hivyo, Kyiv bado ina uhakika wa kushinda. "Kidogo kidogo, tunawalazimisha wavamizi kuondoka katika ardhi yetu," Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema Jumamosi, akikiri hata hivyo kwamba "hali ya Donbass bado ni ngumu. Wanajeshi wa Urusi wanajaribu kupata angalau ushindi huko."

Nchi za NATO zitaendelea kuisaidia Ukraine kijeshi, imebainisha Berlin huku Finland ikitangaza kuzania nafasi ya uenyekiti katika Muungano wa Atlantiki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.