Pata taarifa kuu

Zelensky: Rais Emmanuel Macron ni mpatanishi mkubwa kati yetu na Urusi.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anasema anaamini mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron, anajaribu bila mafanaikio  kufanya mazungumzo na Vladimir Putin wa Urusi kuhusu vita vinavyoendelea

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron. Aurelien Morissard/IP3 - Aurelien Morissard
Matangazo ya kibiashara

Rais Zelensky ameiambia Televisheni ya Italia, Rai 1, kuwa jitihada za rais Macron zinaonekana kutozaa matunda.

Kauli hii inakuja, wakati huu Urusi ikisema, haitakubali mazungumzo ya kumaliza vita vinavyoendelea, hadi pale itakapotaka kufanya hivyo.

Aidha, imebainika kuwa, rais Macron hajawahi kuzungumza chochote na Putin bila ya rais Zelensky, kutaarifiwa kinachoendelea.

Katika hatua nyingine, Ufaransa imesema mataifa ya G 7 yameapa kuendelea kuwa nyuma ya Ukraine, wakati huu Uingereza ikitaka silaha zaidi kusafirishwa jijini Kiev.

Aidha, Mkuu wa sera ya mambo ya nje ya Umoja wa Ulaya, Joseph Borell ameahidi kuwa, Umoja huo utatoa Euro Milioni 500 kama usaidizi kwa jeshi la Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.