Pata taarifa kuu

Ufaransa kuondoa ulazima wa kuvalia barakoa katika usafiri wa umma: Mei 16.

Waziri wa afya nchini Ufaransa Olivier Veran , ametangaza kuwa raia nchini humo kuaanzia Mei 16 hawatahitajika kuvalia barakoa wakati watakapokuwa wakitumia usafiri wa treni na ndege.

 Olivier Veran,Waziri wa afya nchini Ufaransa.
Olivier Veran,Waziri wa afya nchini Ufaransa. © Thomas Coex via AP
Matangazo ya kibiashara

Sheria hiyo ya uvaaji barakoa katika maeneo ya usafiri ndio sheria peke iliyokuwa imesalia nchini humo katika vita dhidi ya msambao wa uviko 19  tangu kutangazwa kwa janaga hilo mwaka wa 2020.

Sheria kuhusu uvaaji barakoa iliaanza kulegezwa nchini Ufaransa mwezi Feburuari  baada ongezeko la maambukizi kushuhudiwa katika kipindi cha msimu wa baridi japokuwa zilihitajika kutumika shuleni na maeneo ya kazi  kwa majuma kadhaa hadi wakati ambapo maambukizi yalipopungua.

Licha ya agizo hilo , raia bado wanatakiwa kuvalia barakoa wanapokuwa katika maeneo ya hosipitali .

Asilimia 79.3 ya raia nchini Ufaransa tayari wamepokea dozi zote za chanjo ya uviko 19 kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya afya nchini humo.

Baadhi ya mataifa duniani yamekuwa yakilegeza sheria za kupambana na msambao wa uviko 19,Mataifa ya bara Afrika yakiwemo Kenya yameondoa sheria hizo ikiwemo ulazima wa uvaaji barakoa.

Shirika la afya duniani WHO limekuwa likitoa wito kwa raia kote duniani kupata chanjo ya uviko 19 ilikumaliza janaga hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.