Pata taarifa kuu

Kyiv yadai kuwa maelfu wa askari wake bado wako Azovstal

Katika siku ya 76 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Rais wa Urusi Vladimir Putin siku ya Jumatatu alihalalisha uvamizi wa Ukraine dhidi ya "tishio lisilokubalika" lililochochewa na jirani yake anayeungwa mkono na nchi za Magharibi, mbele ya maelfu ya wanajeshi wa Urusi waliokuwa wakiandamana kwenye eneo la Red Square huko Moscow kuadhimisha kumbukumbu ya ushindi wa mwaka wa 1945 dhidi ya utawala wa Kinazi wa Ujerumani.

Moshi juu yakiwanda kikubwa cha Azovstal, ngome ya mwisho ambayo bado iko mikononi mwa wapiganaji wa Ukraine, huko Mariupol, Mei 8, 2022.
Moshi juu yakiwanda kikubwa cha Azovstal, ngome ya mwisho ambayo bado iko mikononi mwa wapiganaji wa Ukraine, huko Mariupol, Mei 8, 2022. REUTERS - ALEXANDER ERMOCHENKO
Matangazo ya kibiashara

Mapigano yalishika kasi siku ya Jumatatu mashariki na kusini mwa Ukraine. "Vita vikali vinaripotiwa karibu na miji ya Rubizhne na Bilohorivka" katika mkoa wa Luhansk, Gavana Serhyi Gaidai amesema.

Makombora pia yamelenga eneo la Odessa, jeshi la Ukraine likihesabu mashambulio saba na kubaini kwamba mtu mmoja ameuawa na watano kujeruhiwa. Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel, katika ziara ya ghafla katika jiji hili kubwa la kusini, alilazimika kwenda katika eneo salama.

"Urusi ilikuwa inakabiliwa na tishio lisilokubalika kabisa," Vladimir Putin alisema kuhalalisha uvamizi dhidi ya Ukraine wakati wa hotuba yake wakati wa kumbukumbu ya ushindi dhidi ya utazala wa Kinazi wa Ujerumani mnamo mnamo 1945.

Badala ya kyiv kujiunga na EU ambayo ingechukua "miongo kadhaa", Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amependekeza kuundwa kwa "jumuiya ya kisiasa ya Ulaya" ambayo inaweza kuunganisha Ukraine na "mataifa mengine ya Ulaya ambayo yako chini ya mfumo wa kidemokrasia yanayofuata maadili yetu ya msingi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.