Pata taarifa kuu

Urusi yafanya kumbukizi ya vita ya pili vya dunia.

Urusi,  inasherekea ushindi wake wa mwaka 1945 dhidi ya utawala wa kinazi wa Ujerumani kwa kuonyesha gwaride ya zani zake za kijeshi maadimisho yanayokuja wakati huu ambapo Moscow inaendeleza mashambulio mashariki mwa Ukraine  watu 60 wakiuwawa katika shambulio la angani katika shule moja iliyokuwa inatumika kama hifadhi kwa raia wa taifa hilo wanatoroka mapigano.

Zana za kivita za jeshi la Urusi.
Zana za kivita za jeshi la Urusi. REUTERS - MAXIM SHEMETOV
Matangazo ya kibiashara

Rais Vladimir Putin, anatarajiwa kuongoza halfa hiyo katika siku hii ambayo imetajwa kuwa ya umuhimu mkubwa kwa Urusi, Putin akitumia hafla hii kudhibitishia umma sababu ya uvamizi wake dhidi ya Ukraine kuchukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa.

Maadimisho haya yanajiri wakati huu ambapo rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, akidhibitisha kuwawa kwa raia 60 katika shambulio la anga ambalo limetekelezwa na Moscow kwenye shule moja mashariki mwa mji wa Bilogorivka.

Shambulio hili la hivi punde katika ardhi ya Ukraine, limetajwa kuwa kubwa zaidi kutekelezwa na Urusi tangu taifa hilo kulivamia taifa huru la Ukraine tarehe 24 ya mwezi feburuari.

Kitendo cha Urusi kimekashifiwa vikali na Katibu mkuu wa umoja wa mataifa UN, Antonio Guterres ambaye anataka Moscow kutowashambulia raia wasio na hatia wakati wakati wa mapigano.

Mamlaka nchini Ukraine imesema itatangaza idadi kamili ya watu waliofariki katika shambulio hilo baada ya kukamilisha shughuli ya kuwaondoa watu waliokwama kwenye mabaki ya jumba liloshambuliwa kwa mabomu ya Urusi.

Hili likiwa Shambulio la hivi punde kutekelezwa na Urusi kwa Ukraine, Shughuli ya kuwaondoa watu katika kiwanda cha kutengeza vyuma cha Azovstal jijini Mariupol kilichoshambuliwa awali na Urusi, kusini mashariki mwa Ukraine ikiwa inaendelea ambapo mabasi yaliowabeba raia wa Ukraine yameonekana yakiwasili katika mji unaotawaliwa na Ukraine wa Zaporizhzhia, imesema ripoti ya UN.

Matukio haya yanakuja wakati huu ambapo Jill Biden, mke wa rais wa Marekani Joe Biden akiwa amekikutana na mwenzake wa Ukraine Olena Zelenska nchini Ukraine, Washington nayo yenyewe ikitangaza vikwazo zaidi kwa Moscow.

Hii ni mara ya kwanza kwa Olena Zelenska kuonekana kwenye umma tangu taifa lake kushambuliwa mwezi feburuari, Mkutano kati ya wawili hao umefanyika katika shule moja nchini Ukraine inayotumika kama eneo la kutoa hifadhi ya muda kwa raia ambao makazi yao yameharibiwa katika   mapigano yanayoendelea.

Jill Biden, amesema amefanya ziara nchini Ukraine kama njia moja ya kuonyesha ulimwengu kwa Marekani inasimama na taifa hilo ambapo ametaka urusi kusitisha mashambulizi yake dhidi ya Ukraine, vita ambavyo vimedumu kwa miezi mitatu sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.