Pata taarifa kuu
BELARUS - SIASA

Mahakama nchini Belarus yamfunga jela mwanafunzi Sofia Sapega .

Mahakama nchini Belarus, imemfunga jela miaka sita Sofia Sapega, mwanafunzi na raia wa Urusi hukumu inayokuja ikiwa imepita mwaka moja baada yake na mchumba wake ambaye ni mwanahabari kuondolewa kwenye ndege iliyomilikiwa na shirika la ndege la Ryanair na baadae kukamatwa.

Ndege ya shirika la Ryanair
Ndege ya shirika la Ryanair AP - Mindaugas Kulbis
Matangazo ya kibiashara

Sofia Sapega na mchumba wake Roman Protasevich, walikuwa safarini kuelekea Lithuania wakati ndege yao ilipolazimishwa kubadili mkondo na kuelekea jijini Minsk.

Tukio ambalo lilikashifiwa vikali kote duniani ambapo pia vikwazo vipya vilitangazwa dhidi ya serikali ya rais Alexander Lukashenko.

Mahakama katika uwamuzi wake ilisema ilimpata Sofia Sapega na kosa la kuchochea na kusabisha mgawanyiko.

Awali alikuwa ametuhumiwa na mamlaka nchini Belarus kwa kosa la kupanga maandamano kwenye baadhi ya maeneo nchini humo.

Protasevich, alikuwa akihudumu kama mhariri wa mtandao wa habari wa  Nexta Telegram channel, wenye makao yake nchini Poland, mtandao uliochapisha video na taarifa kuhusu maandano ya mwaka wa 2020 dhidi ya utawala wa rais Lukashenko .

Maandamano makubwa yalifanyika nchini Belarus baada ya Lukashenko kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi wa urais, Uchaguzi ambao wapinzani wake walisema ulikumbwa na hitilafu.

Madai ambayo rais Lukashenko alipinga ambapo alitanagaza msako mkali dhidi ya wapinzani wake, baadhi wakikamatwa na kufungwa jela wengine wakiliazimika kutoroka nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.