Urusi yasema inasitisha vita kwa siku tatu katika eneo la kiwanda cha Azovstal
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametoa wito kwa Umoja wa Mataifa kusaidia kuokoa maisha ya raia wa nchi hiyo waliojeruhiwa na wanaosalia katika kiwanda kikubwa cha kutengeza vyuma katika eneo la Azovstal, mjini Mariupol.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Zelensky ametoa wito huo baada ya kuzungumza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress kwa njia ya simu baada ya baadhi ya watu kuokolewa.
Urusi imesema itasitisha mashambulio katika êneo hilo kwa siku tatu zijazo ili kuwaruhusu raia waliokwama kupelekwa katika maeneo salama.
Matukio ya msingi kuhusu mzozo unaoendelea:
-Vita vimesitishwa katika eneo la Azovstal kwa siku tatu, kuwaruhusu watu kukimbilia katika maeneo salama.
-Ukraine inasema watu zaidi ya 300 wameondolewa kutoka mjini Mariupol siku Jumatano, maisha ya wengine waliosalia yapo hatarini.
-Urusi inasema, jeshi lake limefanya mazoezi ya kurusha makombora ya nyuklia, katika Bahari ya Baltic, iliyo kati ya nchi ya Poland na Lithuania.
-Rais wa Marekani Joe Biden amesema yupo tayari kuiwekea Urusi vikwazo zaidi na atajadiliana na viongozi wenzake kutoka nchi tajiri za G7.
-Ukraine, inaishtumu Urusi kwa kupanag kuwa na gwaride la kijeshi katika mji wa Mauripol, Mei 9, siku ambayo Moscow inakumbuka ushindi dhidi ya wapiganaji wa Kinazi baada ya vita vya pili vya dunia.
-Ripoti zinasema, taarifa za Kiinteljensia, zilizotolewa kwa jeshi la Ukraine kutoka kwa Marekani, zilisaidia wanajeshi wa Ukraine kuwashambulia na kuwauwa Majenerali angalau 12 wa Urusi.