Pata taarifa kuu

Ufaransa: Macron kutawazwa kama rais wa Ufaransa Mei 7

Baada ya ushindi wake wa katika uchaguzi wa urais mnamo Aprili 10 na 24, Emmanuel Macron atatawazwa rasmi kwa muhula wa pili kama mkuu wa nchi Jumamosi Mei 7, 2022. Sherehe hiyo itafanyika katika ukumbi wa ikulu ya Élysée, mjini Paris, saa tano mchana saa za Ufaransa.

Rais wa Ufaransa anaye maliza muda wake Emmanuel Macron.
Rais wa Ufaransa anaye maliza muda wake Emmanuel Macron. AP - Christophe Petit Tesson
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na chanzo cha shirika la habari la AFP kutoka ofisi ya rais, sherehe inapaswa kuwa "ya kawaida", "kuhusiana na kanuni za Republican".

Wakati muhula wa sasa wa Emmanuel Macronunamalizika Mei 13, rais aliyechaguliwa tena amechagua kuandaa sherehe yake ya kuapishwa kwa muhula wake wa pili Jumamosi hii, Mei 7 saa 11 mchana, kituo cha Franceinfo kimebain kikinukuu  kwa chanzo cha serikali, kikithibitisha habari kutoka kituo cha RTL.

Rais wa Mahakama ya Katiba atatangaza matokeo rasmi ya duru ya pili ya uchaguzi wa urais wa tarehe 24 Aprili. Baada ya hapo Emmanuel Macron atatoa hotuba na, kufuata desturi, kutoa heshima kwa bendera ya taifa na kwa kikosi cha ulinzi wa Republican.

Sherehe hizi zitakuwa utangulizi wa uteuzi wa Waziri Mkuu mpya na serikali itakayohusika, pamoja na mambo mengine, kwa ajili ya kuongoza uchaguzi wa wabunge tarehe 12 na 19 Juni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.