Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: EU kutangaza vikwazo vipya didi ya Urusi

Katika siku ya 69 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mnamo Jumanne Mei 3, mkuu wa diplomasia ya Ulaya, Josep Borrel, ametangaza kuwa vikwazo vya sita dhidi ya Urusi vinatayarishwa kuchukuliwa, vikilenga sekta za benki na nishati.

Mkuu wa diplomasia ya Ulaya, Josep Borrel, huko Panama, Jumatatu Mei 2, 2022.
Mkuu wa diplomasia ya Ulaya, Josep Borrel, huko Panama, Jumatatu Mei 2, 2022. © Arnulfo Franco, AP
Matangazo ya kibiashara

► Vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Urusi kufuatia uvamizi wake nchini Ukraine havitaondolewa hadi pale Moscow itakapofikia makubaliano ya amani na Ukraine, amesema Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, akiongeza kuwa Ukraine lazima iamue mazingira ya makubaliano haya. Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anatarajia kulihutubia Bunge la Ukraine Jumanne kwa njia ya video.

► Raia mia moja waliweza kuondoka katika kiwanda cha Azovstal huko Mariupol, bandari ya kusini mashariki mwa Ukraine iliyozingirwa na Urusi, siku ya Jumamosi. kyiv inatumai kuwa shuguli ya kuwahamisha raia waliokwama itaweza kuanza tena Jumanne hii.

► Kulingana na hesabu ya hivi punde ya shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi, UNHCR, zaidi ya raia 3,000 wameuawa katika mapigano na mashambulizi ya anga tangu uvamizi wa Ukraine tarehe 24 Februari.

► Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Yair Lapid Jumatatu alikashifu matamshi ya mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov, ambaye alidai kuwa Hitler "ana damu ya Kiyahudi". Mkuu wa diplomasia alikuwa akijaribu kueleza kuwa ukweli kwamba rais wa Ukraine ni Myahudi haupingani na madai ya Moscow kwamba alianzisha uvamizi huo ili "kuiangamiza" nchi.

► Urusi haitaki kumaliza vita nchini Ukraine na tarehe 9 Mei, inaadhimishwa kama siku ya ushindi, kulingana na Sergey Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.