Pata taarifa kuu

Mauaji ya Bucha: Guterres atoa wito kwa Moscow kushirikiana na ICC

Baada ya mkutano wake na Vladimir Putin mjini Moscow, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres yuko nchini Ukraine Alhamisi hii, Aprili 28. Asubuhi, Antonio Guterres alikwenda kwenye vitongoji vya Kyiv, kwenye miji mitatu iliyokumbwa na zimwi la mauaji yanaohusishwa jeshi la Urusi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizuru mji wa  Irpin, Aprili 28, 2022.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizuru mji wa Irpin, Aprili 28, 2022. REUTERS - GLEB GARANICH
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya kwanza ya ziara ya Antonio Guterres ilikuwa Borodianka Alhamisi hii. Mji huu uliharibiwa na milipuko ya mabomu ambapo maiti nyingi za raia ziligunduliwa baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa Urusi. "Vita haina nafasi katika karne ya 21," Antonio Guterres amesema, mbele ya nyumba zilizoharibiwa.

Vita katika karne ya 21 havina nafasi, havikubaliki. Hapa, naiwazia familia yangu, katika mojawapo ya nyumba hizi zilizoharibiwa na nyeusi. Namuona mjukuu wangu anakimbia kwa hofu. Sehemu ya familia ambayo iliishia kuuawa.

Kisha amezuru eneo lingine ambalo limekuwa ishara ya ukatili uliofanywa tangu uvamizi wa Urusi, Bucha, ambapo Umoja wa Mataifa umeorodhesha mauaji ya raia wasiopungua 50, wengine kwa kunyongwa kkikatili.

"Akiwa na huzuni, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezungumza na waandishi wa habari: "Tunapoona eneo hili la kutisha, ninatambua jinsi ilivyo muhimu [kuwa na] uchunguzi wa kina na uwajibikaji. Ninafurahi kwamba mahakama ya Ukraine inaona hali hii, na kwamba ofisi ya mwendesha mashitaka iko tayari kuanzisha uchunguzi. Ninaunga mkono kikamilifu Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) na ninatoa wito kwa Shirikisho la Urusi kukubali, kushirikiana na ICC. Lakini tunapozungumzia uhalifu wa kivita, hatuwezi kusahau kwamba uhalifu mbaya zaidi ni vita yenyewe. "

Na "siku zote ni raia wanaopata hasara kubwa zaidi," Antonio Guterres amesema wakati wa hatua yake ya tatu, huko Irpin. Kyiv Inashutumu vikosi vya Urusi kwa kufanya mauaji huko pia. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atapata fursa ya kujadili hili na Rais Volodymyr Zelensky leo mchana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.