Pata taarifa kuu

Nchi 40 zaungana kwa kuimarisha ulinzi wa Ukraine

Kwa siku ya 62 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Zaidi ya nchi 40 zinakutana nchini Ujerumani ili kuongeza mchango wao wa silaha kwa Ukraine, huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi akionya juu ya hatari ya mzozo huo kugeuka na kuwa vita vya tatu vya dunia.

Wanajeshi wa Ukraine wakipakia makombora kwenye lori , silaha zilizotolewa na Marekani kama sehemu ya usaidizi wa kijeshi unaoendelea, katika uwanja wa ndege wa Boryspil mjini Kyiv, Ukraine, Februari 11, 2022.
Wanajeshi wa Ukraine wakipakia makombora kwenye lori , silaha zilizotolewa na Marekani kama sehemu ya usaidizi wa kijeshi unaoendelea, katika uwanja wa ndege wa Boryspil mjini Kyiv, Ukraine, Februari 11, 2022. AFP - SERGEI SUPINSKY
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Pentagon Lloyd Austin alisema siku ya Jumatatu kuwa Ukraine inaweza kushinda vita hivyo, siku moja baada ya ziara ya kwanza ya viongozi wa Marekani mjini Kyiv tangu uvamizi wa Urusi. "Wanaweza kushinda ikiwa wana vifaa vinavyofaa, usaidizi unaofaa," Lloyd Austin alisema baada ya kukutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, akiambatana na Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken.

► Urusi imehakikisha kwamba inataka kuendeleza mazungumzo ya amani na Ukraine, huku ikionya juu ya hatari "halisi" kwamba mzozo huo utageuka na kuwa vita vya tatu vya dunia, siku moja baada ya ziara ya mawaziri wa Marekani huko Kyiv.

► Urusi Jumatatu usiku ilishutumu mamlaka ya Ukraine kwa kuwazuia raia wanaoshikiliwa na wapiganaji wa Ukraine katika jumba la madini la Azovstal lililoko Mariupol, kusini mashariki mwa Ukraine, kuondoka katika maeneo hayo, licha ya tangazo la kusitishwa kwa mapigano na jeshi la Urusi.

► Idadi ya wakimbizi wanaokimbia uvamizi wa Urusi inazidi milioni 5.2, kulingana na Umoja wa Mataifa. Zaidi ya watu milioni 7.7 wametoroka makazi yao lakini bado wako Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.