Pata taarifa kuu

Marekani yakubali kuipa Ukraine msaada wa dola Milioni 700

Nchini Ukraine, wanajeshi wa Urusi wanapoendelea kuvamia eneo la nchi hiyo, Marekani imeahidi msaada zaidi wa kijeshi, wa Dola Milioni 700.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky 23 Aprili, 2022.
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky 23 Aprili, 2022. AP - Efrem Lukatsky
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken na Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin wametoa ahadi hiyo baada ya kuzuru Kiev na kukutana na rais Volodymyr Zelenskyy. 

Blinken anasema, licha ya Urusi kuharibu na kutekeleza mauji ya rais, inapoteza vita hivyo. 

Katika hatua nyingine rais wa Urusi, Vladimir Putin ameyashtumu mataifa ya Magharibi kwa kujaribu kuiharibu nchi yake na kujaribu kuumuua mwanahabari mashuhuri, jaribio ambalo amesema halitafanikiwa. 

Aidha, Wizara ya Ulinzi imetangaza kusitisha mapigano katika eneo la kiwanda cha vyuma cha Azovstal mjini Mariupol ili kuruhusu raia kukimbilia katika maeneo salama. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.