Pata taarifa kuu

Emmanuel Macron: Niko tayari kulitumikia taifa kwa maslahi ya raia wote

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, baada ya kuchaguliwa tena kuongoza nchi hiyo kufuatia ushindi dhidi ya mpinzani wake Marine Le Pen, ameapa kuanza kazi ngumu ya kuliunganisha taifa hilo lililogawanyika kisiasa.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron asherehekea ushindi wake na wafuasi wake mjini Paris, Ufaransa, Jumapili, Aprili 24, 2022.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron asherehekea ushindi wake na wafuasi wake mjini Paris, Ufaransa, Jumapili, Aprili 24, 2022. AP - Thibault Camus
Matangazo ya kibiashara

Macron aliyepata ushindi wa asilimia 58.54 dhidi ya Le Pen aliyepata asilimia 41.46, amesema atakuwa rais wa wote. 

Licha ya kushindwa, Le Pen amesema chama chake kimeshinda na sasa nguvu zinaelekezwa kwenye uchaguzi wa wabunge mwezi Juni. 

Macron anakuwa rais wa kwanza kuchaguliwa kwa mihula miwili nchini Ufaransa, baada ya miaka 20.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.