Pata taarifa kuu

Wapiganaji wa Ukraine waomba ‘dhamana ya usalama’ kuondoka Mariupol

Katika siku ya 57 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Kyiv siku ya Jumatano ilitoa wito kwa mazungumzo na Urusi juu ya hatima ya mji unaozingirwa wa Mariupol, wakati ambapo Moscow ilionyesha nguvu zake kwa kufanya majaribio ya kombora jipya la masafa marefu.

Moshi mweusi juu ya kiwanda cha Azovstal huko Mariupol, Aprili 20, 2022.
Moshi mweusi juu ya kiwanda cha Azovstal huko Mariupol, Aprili 20, 2022. REUTERS - ALEXANDER ERMOCHENKO
Matangazo ya kibiashara

Ukraine imetoa wito wa mazungumzo ya haraka na Urusi mjini Mariupol, mji unaokaribia kutekwa baada ya wiki kadhaa za uvamizi wa Urusi huku Rais Vladimir Putin akiendelea kujipiga kifua na kuonyesha uwezo wake wa kijeshi.

Wakati huo huo Urusi imeionya rasmi Marekani - na mataifa mengine washirika dhidi ya kusambaza silaha kwa Ukraine.

Onyo hilo lilikuja katika barua rasmi ya kidiplomasia kutoka Moscow, ambayo nakala yake imepitiwa na vyombo vya habari nchini Marekani.

Wakati kuanguka kwa Mariupol kunaonekana kuwa karibu na hali ni muhimu kwa wakazi wake wa mwisho na watetezi, Mykhaïlo Podolyak, mshauri wa rais wa Ukraine na mmoja wa wapatanishi na Urusi, amependekeza Moscow "kikao maalum cha mazungumzo" katika mji wa bandari, kwenye Bahari ya Azov iliyozingirwa.

Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel, akizuru Kyiv, alihakikishia Jumatano kwamba Umoja wa Ulaya utafanya "kila linalowezekana" kwa Ukraine "kushinda vita" dhidi ya Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.