Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Urusi yawawekea vikwazo Wamarekani 90, akiwemo Kamala Harris

Katika siku ya 57 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Vladimir Putin amebaini kwamba vikosi vyake "vimefanikiwa" kuukomboa mji wa Mariupol na kuagiza kuwazingira wapiganaji waliosalia wa Ukraine badala ya kuwavamia.

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris amech na Urusukuliwa vikwazo pamoja na Wamarekani wengine 89 na Wacanada, Alhamisi hii, Aprili 21, 2022.
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris amech na Urusukuliwa vikwazo pamoja na Wamarekani wengine 89 na Wacanada, Alhamisi hii, Aprili 21, 2022. AP - Jacquelyn Martin
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Urusi ametoa wito kwa vikosi vyake "kuziba eneo hili la viwanda ili hata inzi asitoroke".

Ameongezea haiteleweka kuvamia eneo kubwa lenye viwanda , ambapo zaidi ya wanajeshi 2000 wa Ukraine wanaripotiwa kuwepo na kwamba uamuzi huo ulikuwa unafanywa kulinda usalama wa wanajeshi wa Urusi.

Putin amewasifu wanajeshi wa Urusi kwa ‘kuuweka huru’ mji wa Mariupol baada ya waziri wa ulinzi Sergei Shoigu kumwambia kwamba wanajeshi wa taifa hilo wanadhibiti mji huo wa bandari wa Ukraine ijapokuwa bado kuna makabiliano kukiteka kiwanda hicho.

Wakati huo huo Urusi imepiga marufuku kuingia katika eneo lake kwa raia 90 kutoka Amerika Kaskazini wakiwemo Mark Zuckerberg na Kamala Harris. Kwa upande wake, London imepanua vikwazo vyake dhidi ya Urusi, huku ikipiga marufuku uagizaji wa fedha, bidhaa za mbao na bidhaa za hali ya juu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.