Pata taarifa kuu

Kyiv yadai haraka kutengwa kwa maeneo ya usalama wa kiutu wa Azovstal, Mariupol

Rais wa Urusi Vladimir Putin siku ya Alhamisi amedai kukombolewa kwa mji wa Mariupol, akisema amefuta mpango wake wa kuvamia kiwanda cha vyuma cha Azovstal, ambapo wanajeshi wa mwisho wa Ukraine katika mji huo bado walikuwa wakipinga mashambulizi ya Urusi.

Watu wa kujitolea wajifunza matumizi ya bunduki kwenye kambi ya mafunzo nchini Ukraine.
Watu wa kujitolea wajifunza matumizi ya bunduki kwenye kambi ya mafunzo nchini Ukraine. © RFI / Oriane Verdier
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano, Mykhaïlo Podolyak, mshauri katika ofisi ya rais Ukraine na mmoja wa wapatanishi na Urusi, alikuwa amependekeza kwa Moscow "kikao maalum cha mazungumzo" katika mji wa bandari kwenye Bahari ya Azov.

Alhamisi wiki hii Kyiv ilitoa wito wa kuanzishwa kwa maeneo ya usalama ya kiutu ili kuwahamisha raia waliowekwa katika kiwanda kikubwa cha Azovstal huko Mariupol. Baada ya siku nne bila ya watu kuhamishwa, mabasi manne ya raia yamefanikiwa kuondoka kwenye bandari ya Mariupol, Naibu Waziri Mkuu wa Ukraine Iryna Vereshchuk amesema Alhamisi asubuhi.

Zaidi ya miili ya 1,000 ya watu waliouawa kwa sasa iko katika vyumba vya kuhifadhia maiti katika mkoa wa Kyiv, kulingana na afisa wa Ukraine, huku kyiv ikiishutumu Urusi kwa 'kuua' mamia ya raia wakati wa uvamizi wake katika eneo hilo mwezi Machi, jambo ambalo Moscow inakanusha

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.