Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Volodymyr Zelensky aedelea kushushia lawama Urusi

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anasema, uharibufu unaoshuhudiwa katika mji wa Borodianka ni mkubwa ikilinganishwa na kile ambacho kimekuwa kikijiri katika mji wa Bucha, ulioshuhudia mauaji ya mamia ya watu.

Rais Volodymyr Zelensky akizuru mji wa Bucha, kaskazini-magharibi mwa mji mkuu wa Ukraine wa Kyiv, Aprili 4, 2022. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema Aprili 3, 2022 kwamba viongozi wa Urusi walihusika na mauaji ya raia huko Bucha, nje ya Kyiv, ambapo miili ilipatikana ikiwa imetapakaa barabarani baada ya jeshi la Ukraine kuuteka mji huo.
Rais Volodymyr Zelensky akizuru mji wa Bucha, kaskazini-magharibi mwa mji mkuu wa Ukraine wa Kyiv, Aprili 4, 2022. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema Aprili 3, 2022 kwamba viongozi wa Urusi walihusika na mauaji ya raia huko Bucha, nje ya Kyiv, ambapo miili ilipatikana ikiwa imetapakaa barabarani baada ya jeshi la Ukraine kuuteka mji huo. © AFP - RONALDO SCHEMIDT
Matangazo ya kibiashara

Rais Zelensky amesema, hali ya mambo katika mji wa Borodianka itakavyofahamika, dunia itastajabishwa. 

Aidha kiongozi huyo wa Ukraine, amesema kwa sasa kinachoendelea kwa sasa ni shughuli za kuusafisha mji huo. 

Wakati hayo yakijiri, viongozi wa Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen na Josep Borrell watazuru jijini Kiev kukutana na rais Zelensky.

Hii inakuja baada ya Umoja wa Ulaya kukubaliana kupiga marufuku uingizwaji wa makaa ya mawe kutoka nchini Urusi; 

Wabunge nchini Marekani nao wamepigia kura kuzuia uingizwaji wa mafuta kutoka Urusi, na kufuta kauli kuwa, Urusi ni mshirika wake wa karibu inapokuja kwenye suala la kufanya biashara. 

Jeshi la nchi za Magharibi NATO, limesema litaendelea kuipa Ukraine silaha, kujilinda dhidi ya mashambulio ya Urusi. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.