Pata taarifa kuu

NATO kupeleka vikosi vipya Bulgaria, Romania, Hungary na Slovakia

Washirika thelathini wa NATO watakutana Alhamisi hii, Machi 24 katika mkutano wa dharura ambao utakuwa wa kwanza kati ya mikutano mitatu ya kilele ya Brussels kabla ya mkutano wa G7 na ule wa EU.

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg, katika siku moja kabla ya mkutano wa kilele wa Umoja huo, mjini Brussels, Jumatano, Machi 23.
Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg, katika siku moja kabla ya mkutano wa kilele wa Umoja huo, mjini Brussels, Jumatano, Machi 23. REUTERS - GONZALO FUENTES
Matangazo ya kibiashara

Washirika hao watazungumza juu ya kuimarishwa kwao Mashariki na uungaji mkono wa moja kwa moja kwa Ukraine, lakini hawataki kusababisha kuongezeka kwa ghasia na kuishia na ushiriki wa NATO katika mzozo huo, ambao ungesababisha athari zisizoweza kuhesabika.

Miongoni mwa maamuzi ambayo washirika thelathini wa NATO watalazimika kufanya katika mkutano huo ni kuongezwa kwa wanajeshi wa NATO katika upande wake wa mashariki. Muungano huo umeweka bataliani vinne ya wanajeshi katika nchi za Baltic na Poland tangu Crimea kudhibitiwa kutoka mikononi mwamajeshi ya Ukraine. Ukubwa wa vita hivi umeongezwa maradufu na idadi yao pia itaongezeka maradufu kwa kuwekwa kwa bataliani nne za vikosi vipya katika nchi washirika jirani na Ukraine: Bulgaria, Romania, Hungary na Slovakia, meripoti mwandishi wetu huko Brussels, Pierre Benazet.

"Hatutatuma wanajeshi washirika nchini Ukraine, lakini bado tunajiimarisha," amesema Jens Stoltenberg, Katibu Mkuu wa NATO.

Na wanajeshi hawa watakuwa moja ya nguzo za uimarishaji wa muda mrefu wa NATO dhidi ya Urusi. ujihami wa NATO.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.