Pata taarifa kuu

Wajumbe wa Umoja wa Ulaya wazuru Ukraine katikati mwa vita

Viongozi wawili wa Umoja wa Ulaya, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Czech, na viongozi wa Poland na Slovenia wanatarajiwa kuzuru Ukraine, wakati huu Urusi inapoendelea kutekeleza mashambulizi yake katika nchi hiyo jirani. 

Eneo moja la Mashariki mwa mji wa Marioupol lashambuliwa, Machi 14, 2022.
Eneo moja la Mashariki mwa mji wa Marioupol lashambuliwa, Machi 14, 2022. via REUTERS - MAXAR TECHNOLOGIES
Matangazo ya kibiashara

Haya yanajiri wakati huu Meya wa mjin wa Kyiv Vitali Klitschko akitanagaza makataa ya saa 35 ya watu kutotembea katka mji huo mkuu, huku wanajeshi wa Urusi wakiendeleza mashambulizi yao. 

Hatua hii imekuja baada ya wanajeshi wa Urusi kushambulia kituo cha usafiri wa umma na majengo ya wakaazi a kusababisha vifo vya watu wanne. 

Wakati huo huo, magari madogo Elfu mbili yameondoka katika mji wa Mariupol, yakiwa na watu wanaotoroka mashambulizi. 

Katika hatua nyingine, nchi za Magharibi zinazounda umoja wa jeshi la NATO, zimeonya kuwa, iwapo mwanachama wake atashambuliwa na Urusi, jeshi hilo litajibu. 

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema jeshi hilo linachunguza iwapo China inatoa msaada wa Urusi. 

Mpaka sasa zaidi ya watu Milioni tatu wamekimbia nchini Ukraine kwa mujibu wa Umojaa wa Mataifa, miongoni mwao Milioni moja na Laki Nane wakikimbilia nchini Poland. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.