Pata taarifa kuu

Volodymyr Zelensky akiri kwamba nchi yake haitaweza kujiunga na NATO

Katika siku ya ishirini ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, vitongoji kadhaa katikati mwa mji wa Kyiv vimekumbwa na mashambulizi ya anga ya Urusi wakati duru ya nne ya mazungumzo imeanza tena Jumanne (Machi 15). Ni katika muktadha huu ambapo Mawaziri Wakuu wa Poland, Czech na Slovenia wanazuru Kyiv.

Mashambulio kadhaa yameripotiwa katikati mwa Kyiv mnamo Jumanne Machi 15, 2022.
Mashambulio kadhaa yameripotiwa katikati mwa Kyiv mnamo Jumanne Machi 15, 2022. AP - Justin Tallis
Matangazo ya kibiashara

Pointi kuu:

► Vitongoji kadhaa katikati mwa mji w Kyiv vimelengwa na mashambulizi ya anga ya jeshi la Urusi na angalau watu wanne wameuawa. Sheria ya kutotoka nje kwa saa 36 imetangazwa kuanzia Jumanne jioni.

► Duru ya nne ya mazungumzo kati ya Urusi na Ukraine imeanza tena Jumanne baada ya siku ya kwanza ya majadiliano kwa njia ya video siku ya Jumatatu.

► Mawaziri Wakuu wa Poland, Czech na Slovenia wanazuru mji wa Kyiv kuonyesha "uungaji mkono usio na shaka" wa Umojawa Ulaya, EU, kukutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

► "Lazima ifahamike" kwamba Ukraine haitaweza kujiunga na NATO, amesema Volodymyr Zelensky, kwa mkutano wa video wakati wa mkutano wa viongozi wa nchi za Kikosi cha Pamoja cha Joint Expeditionary Force, muungano unaoongozwa na Uingereza.

► Zaidi ya watu milioni 3 wameikimbia Ukraine tangu Februari 24, kulingana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.