Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Sheria ya kutotoka nje katika mji wa Kyiv kuanza kutumika

Katika siku ya ishirini ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, vitongoji kadhaa katikati mwa Kyiv vilikumbwa na mashambulizi wakati duru ya nne ya mazungumzo ilianza tena Jumanne (Machi 15). Ni katika muktadha huu ambapo Mawaziri Wakuu wa Poland, Jamhuri ya Czech na Slovenia wanatarajia kuzuru mji wa Kyiv.

Mashambulio kadhaa yameripotiwa katikati mwa Kyiv Jumanne Machi 15, 2022.
Mashambulio kadhaa yameripotiwa katikati mwa Kyiv Jumanne Machi 15, 2022. AP - Felipe Dana
Matangazo ya kibiashara

Pointi kuu:

► Vitongoji kadhaa katikati mwa mji wa Kyiv vimelengwa na mashambulizi ya anga ya Urusi na angalau watu wawili waliokolewa kutoka kwa vifusi vya majengo yaliyokumbwa na mashambulizi anga ya ndege za Urusi Jumanne asubuhi. Sheria ya kutotoka nje kwa saa 35 imetangazwa kuanzia leo Jumanne jioni.

► Mawaziri Wakuu wa Poland, Jamhuri ya Czech na Slovenia watafanya ziara katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, leo Jumanne kuonyesha "uungaji mkono usio na shaka" wa Umoja wa Ulaya, EU, kukutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

► Maeneo ya usalama wa kiutu yatafunguliwa kuanzia saa moja asubuhi saa za kimataifa ili kuhamisha watu kutoka miji ya Sumy, Konotop, Trostianets na Lebedine. Jumatatu, baadhi ya magari 160 yaliweza kuondoka katika jiji la Mariupol, unaoendelea kuzingirwa na kushambuliwa kwa mabomu kwa karibu wiki mbili.

► Duru ya nne ya mazungumzo kati ya Urusi na Ukraine imeanza tena Jumanne baada ya siku ya kwanza ya majadiliano kwa njia ya video siku ya Jumatatu.

Kulingana na duru za kuaminika mashambulio ya Urusi yamekaribia sehemu ya kati ya mji mkuu wa Ukraine, Kyiv leo ambapo sehemu kadhaa za makaazi ya raia zimepigwa. Kwa mujibu wa taarifa zaidi shambulio la mzinga lilisababisha moto mkubwa kwenye nyumba ya ghoroga 15. Mtu mmoja ameuawa na wengine kadhaa wamekwama ndani ya jengo hilo. Juhudi kubwa za uokozi zinaendelea.

Kwa upande mwengine kulingana na duru kutoka vyanzo vya usalama vya Ukraine baadhi ya wanajeshi wa Urusi wamekataa kutii amri , ndege zao nne zimeangushwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.