Pata taarifa kuu

Moscow yashutumu Pentagon kwa kufadhili utafiti wa silaha za kibaolojia nchini Ukraine

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imeshutumu Marekani kwa kufadhili mpango wa silaha za kibiolojia nchini Ukraine, ikisema kuwa imepata ushahidi wa hayo katika maabara za Ukraine. "Lengo la utafiti huu wa kibayolojia unaofadhiliwa na Pentagon nchini Ukraine lilikuwa kuunda utaratibu wa kuenea kwa siri kwa vimelea hatari," msemaji wa wizara ya Ulinzi Igor Konashenkov amesema katika taarifa yake ya asubuhi kuhusu mzozo wa Ukraine.

Rais wa Urusi Vladimir Putin huko Moscow.
Rais wa Urusi Vladimir Putin huko Moscow. AP - Alexei Nikolsky
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na afisa huyo, Moscow imepata "nyaraka zilizowasilishwa na wafanyakazi wa maabara ya Ukraine", akimaanisha "uhamishaji wa nyenzo za kibinadamu zilizochukuliwa nchini Ukraine kwenda nchi za nje kwa ombi la wawakilishi wa Marekani". Bw. Konachenkov pia ametaja "mradi wa Marekani juu ya uhamisho wa pathogens na ndege mwitu wanaohama kati ya Ukraine na Urusi na nchi nyingine jirani". Amehakikisha kwamba Marekani ilikuwa inapanga "kuendesha kazi ya pathogens ya ndege na popo nchini Ukraine mwaka wa 2022" na pia juu ya "uwezekano wa kuenea kwa homa ya nguruwe kutoka Afrika na anthrax".

Marekani na Ukraine zimekanusha kuwepo kwa maabara zinazonuiwa kuzalisha silaha za kibiolojia nchini humo. Urusi ilikuwa tayari imeishutumu Marekani mnamo mwaka 2018 kwa kufanya majaribio ya kibaolojia kwa siri katika maabara huko Georgia, jamhuri nyingine ya zamani ya Soviet ambayo, kama Ukraine, inalenga kujiunga na NATO na Umoja wa Ulaya, EU.

Wakati huo huo serikali ya Ukraine imesema itaanzisha hifadhi kubwa ya chakula cha kutosha kuwalisha watu na vikosi vya jeshi wakati huu wa uvamizi wa Urusi.Chombo cha habari cha serikali kimemnukuu Waziri Mkuu Denys Shmgal akisema serikali itakomboa nafaka na akiba zingine kwenye matumizi ya kila mwaka na nchi nzima kwa gharama ya bajeti ya serikali. Ukraine ni mzalishaji mkuu wa kimataifa wa chakula na muuzaji wa nje

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.