Pata taarifa kuu

Mkutano muhimu kufanyika kati ya Mawaziri wa mambo ya nje wa Urusi na Ukraine

Katika siku ya kumi na tano ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Rais wa Ukraine ametangaza kuwa raia 35,000 wamehamishwa kutoka miji mbalimbali iliyozingirwa siku ya Jumatano kupitia maeneo salama ya kiutu. Kwa upande wa kidiplomasia, mazungumzo kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa Ukraine na Urusi yanatarajiwa kuanza Alhamisi na viongozi wa Umoja wa Ulaya, EU, wanakutana kwa mkutano usio kuwa wa kawaida.

Chini ya daraja lililoharibiwa huko Irpine, Machi 8, 2022.
Chini ya daraja lililoharibiwa huko Irpine, Machi 8, 2022. AFP - SERGEI SUPINSKY
Matangazo ya kibiashara

Pointi kuu:

► Takriban raia 35,000 wamehamishwa kupitia maeneo salama ya kiutu kutoka mji wa Sumy, Enerhodar na maeneo ya karibu na mji mkuu wa Kiev, rais wa Ukraine ametangaza.

► Uturuki inawapokea mawaziri wa mambo ya nje wa Urusi na Ukraine Alhamisi hii. Hii ni mara ya kwanza kukutana katika kiwango hiki tangu kuanza kwa uvamizi mnamo Februari 24. Sergei Lavrov na Dmytro Kuleba wamepokelewa na Waziri wa Uturuki Mevlut Cavusoglu mjini Antalya, kusini mwa nchi hiyo.

► Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanakutana Alhamisi hii huko Versailles katika mkutano usio wa kawaida. Watajadili kupunguza utegemezi wa Ulaya kwa nishati ya Urusi, pamoja na kuimarisha uhusiano na Ukraine.

► Siku tisa za vikosi vya jeshi la Urusi kuzingira mji wa Mariupol, kusini mashariki, hatua ambayo imesababisha jumla ya raia 1,207 kufariki, manispa ya jiji hilo imebaini kwenye kituo chake cha Telegraph. Hospitali ya watoto katika mji huu wa kimkakati wa bandari imeharibiwa na makombora ya Urusi siku ya Jumatano, afisa wa mkoa amesema.

► Kulingana na Umoja wa Mataifa, zaidi ya raia 470 wameuawa na zaidi ya watu milioni 2 wameikimbia Ukraine tangu kuanza kwa mashambulizi ya kijeshi ya Urusi. Miongoni mwao ni watoto milioni moja, kulingana na shirika lisilo la kiserikali la Save The Children. Takriban watu 140,000 waliohamishwa wameongezwa kwenye hesabu katika saa 24 zilizopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.