Pata taarifa kuu

Vita huko Ukraine: Vladimir Putin asema "raia wa Ukarine hawapo"

"Urusi inarejeshwa kwa uadilifu wake wa kihistoria"; sentensi hii imechukuliwa kutoka kwa makala ya shirika la habari la RIA-Novosti ambayo ilichapishwa kimakosa Februari 26 kabla ya kuondolewa baada ya saa chache.Nakala hiyo, ambayo ingeonekana tu baada ya ushindi wa Urusi nchini Ukraine, inaelezea malengo halisi ya vita: sio tu kuhakikisha usalama wa Urusi, lakini pia kurekebisha "kosa la kihistoria" kwa kurudisha Ukraine kwenye mzunguko wake.Kwa upande mwengine Urusi imetangaza usitishwaji mpya wa mashambulizi katika miji ya Ukraine ya Mariupol, Sumy na Kharkiv kuanzia siku ya Jumanne, ili kuwaruhusu raia wa Ukraine kukimbilia maeneo salama, hatua inayotiliwa shaka na uongozi wa Ukraine.Tangazo hili la Urusi linakuja wakati huu Umoja wa Mataifa ukisema watu zaidi ya Milioni 1.7 wameikimbia Ukraine mpaka sasa.Awali,  rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron alishtumu hatua ya Urusi kutotoa nafasi kwa nafasi kwa raia kukimbilia maeneo salama.Wakati hayo yakijiri, rais wa Urusi Vladimir Putin amesema nchi yake haitawatumia raia wa nchi yake waliolazimishwa kuingia jeshini au wanajeshi zaidi wa akiba kuendeleza mashambulizi nchini Ukraine.Mazungumzo kati ya pande mbili yanatarajiwa kuendelea leo.

Rais wa Urusi Vladimir Putin, Desemba 23, 2021.
Rais wa Urusi Vladimir Putin, Desemba 23, 2021. AFP - NATALIA KOLESNIKOVA
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.