Pata taarifa kuu

Urusi yaonywa kuwa itakabiliwa vikali kama itashambulia mmoja wa nchi zinazounda NATO

Mataifa ya nchi za Magharibi yanayounda jeshi la NATO, yanasema yako tayari kupambana na Urusi iwapo, mmoja wa mwanachama wake atashambuliwa.

Raia wa Ukraine wakikimbia uvamizi wa Urusi, wakiwasili, kwenye kituo cha ukaguzi cha polisi kwenye mpaka huko Medyka, Poland, Machi 4, 2022.
Raia wa Ukraine wakikimbia uvamizi wa Urusi, wakiwasili, kwenye kituo cha ukaguzi cha polisi kwenye mpaka huko Medyka, Poland, Machi 4, 2022. REUTERS - YARA NARDI
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka mataifa 30 yanayounda Jeshi hilo wamekuwa wakikutana jijini Brussels, kujadili mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine. 

"Tumesema wazi kuwa hatutahusika na vita hivi kwa kutuma vikosi vyetu ardhini au katika angaa la Ukraine, njia pekee ya kuhakikisha kuwa hakuna ndege inayopaa katika angaa la Ukraine ni kutumia ndege za NATO ili kuzingausha ndege za Urusi, tunaelewa wito wa NATO kuhusika lakini iwapo tutaingilia vita hivi, vitapanuka na kuhusisha nchi nyingi na hivyo kusababisha watu kuteseka, " amesema Anthony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani. 

 Uongozi wa Ukraine umekuwa ukitaka Majeshi ya nchi za Magharibi kufunga angaa lake, lakini hili limekuwa changamoto kwa sababu nchi hiyo sio mwanachama wa NATO. 

Wakati huo huo, NATO imesema itaendelea kuisaidia Ukraine kwa njia nyingine.

Ukraine imekuwa ikitaka Mataifa ya Magharibi kufanya zaidi na kuzuia mashambulizi ya wanajeshi wa Urusi ambao wanaendeleza mashambulizi yao kwa zaidi ya wiki moja sasa. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.