Pata taarifa kuu

Sheria ya kutotoka nje yatangazwa mjini Kiev hadi Jumatatu, raia 198 wauawa kwa siku 3

Siku tatu baada ya kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine siku ya Alhamisi Februari 24, hatima ya Kiev inaonekana kutia mashaka. Mapigano makali yanafanyika katika mji mkuu. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky bado yuko katika mji mkuu. Wakati huo huo, makumi ya maelfu ya watu wa Ukraine wamekimbilia mipakani.

Wanajeshi wa Ukraine wanatafuta na makombora ambayo hayakulipuka baada ya mapigano na kundi la wavamizi la Urusi katika mji mkuu wa Ukraine wa Kiev asubuhi ya Februari 26, 2022.
Wanajeshi wa Ukraine wanatafuta na makombora ambayo hayakulipuka baada ya mapigano na kundi la wavamizi la Urusi katika mji mkuu wa Ukraine wa Kiev asubuhi ya Februari 26, 2022. AFP - SERGEI SUPINSKY
Matangazo ya kibiashara

Pointi kuu:

► Jumamosi hii, macho yameelekezwa kwenye mji mkuu Kiev, ambako mapigano yanaendelea. Rais wa Ukraine ameendelea kusema kuwa yeye ndiye "mlengwa namba moja" wa Moscow. Uhamasishaji wa jumla umeamuliwa kwa upande wa Ukraine. Kwa upande wa Urusi, Wizara ya Ulinzi imetangaza katika taarifa kwa kwamba imetoa amri ya "kupanua mashambulizi".

► Idadi ya muda inaonyesha kuwa raia 198 wameuawa na 1,115 kujeruhiwa. Makmi ya kwa maelfu ya raia wanayatoroka makaazi yao na watu 115,000 wamepata hifadhi nchini Poland, kulingana na ripoti mpya kutoka kwa mamlaka ya Poland.

► Tangu kuanza kwa mashambulizi, vikwazo kadhaa vimechukuliwa kwa mfululizo na Umoja wa Ulaya, Marekani, Uingereza na Canada, zikilenga sekta ya benki, uagizaji wa bidhaa za kiteknolojia na washirika wengi walio karibu na mamlaka. Vikwazo vingine vinamlenga pia Rais wa Urusi Vladimir Putin na Waziri wake wa Mmambo ya Nje Sergei Lavrov.

► Mkutano wa kilele wa NATO ulifanyika Ijumaa. "Tunapeleka Kikosi cha kujihami kwa mara ya kwanza kama sehemu ya ulinzi wa pamoja ili kuzuia mashambulizi kwenye eneo la NATO," amesema Jens Stoltenberg, Katibu Mkuu wa NATO, baada ya mkutano huo. Ufaransa itapeleka wanajeshi 500 nchini Romania kama sehemu ya Muungano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.