Pata taarifa kuu

Ujerumani yasitisha kibali cha bomba la gesi la Nord Stream 2

Baada ya Moscow kutambua uhuru wa majimbo ya Ukraine yanayounga mkono Urusi, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ametangaza kuwa anasitisha uidhinishaji wa bomba la gesi lenye utata linalounganisha Urusi na Ujerumani. Moja ya vikwazo vya kwanza baada ya hotuba ya Vladimir Putin Jumatatu jioni.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz katika mkutano na waandishi wa habari mjini Berlin, Februari 22, 2022.
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz katika mkutano na waandishi wa habari mjini Berlin, Februari 22, 2022. REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kukamilika tu katika msimu wa joto, mradi wa bomba la gesi la Nord Stream 2, ambao haujaanza Kufanya kazi, umezuiwa. Olaf Scholz aMEtangaza Jumanne Februari 22 kusimamisha uidhinishaji wa bomba la gesi la Nord Stream 2, bomba hili la gesi ambalo linaunganisha Ujerumani na Urusi kupitia bomba la zaidi ya kilomita elfu moja chini ya Bahari ya Baltic kwa kuizunguka Ukraine na itaongeza uwezo wa utoaji wa gesi ya Urusi hadi Ulaya.

“Nimeiomba Wizara ya Uchumi kufuta taarifa yake ya usalama wa upatikanaji wa nishati kwenye mamlaka ya udhibiti ili uthibitisho wa kuidhinishwa kwa bomba la gesi usifanyike. Bila kibali hiki, mradi wa bomba la gesi la Nord Stream 2 hauwezi kutumika," amesema Kansela wa Ujerumani, akiongeza kuwa faili "itachunguzwa upya" na serikali ya Ujerumani. Ilikuwa hadi sasa inasubiri kuthibitishwa na mdhibiti wa nishati nchini Ujerumani, kutokana na matatizo ya kisheria, katika kesi hii kutofuata baadhi ya masharti ya sheria za Ujerumani na Ulaya.

Msimamo uliokosolewa

Ujerumani imekuwa ikikosolewa kwa muda mrefu kwa kuunga mkono bomba la gesi la Nord Stream 2, amekumbusha mwanahabari wetu mjini Berlin, Pascal Thibaut. Angela Merkel aliweza kufafanua kama mradi wa kibinafsi usio na historia ya kisiasa. Olaf Scholz alichukua tasnifu hii mwanzoni mwa mamlaka yake kabla ya kujirekebisha. Licha ya yote hayo, kumekuwa na ukosoaji mwingi dhidi ya Berlin katika mzozo wa sasa. Mamlaka ya Ujerumani imekosolewa kwa kutosema wazi kwamba uingiliaji wa Urusi dhidi ya Ukraine utakuwa na athari kwa mradi huo. Wengi wa Wajerumani hivi karibuni walipendelea kuendelea kwa mradi huo. Na maafisa kutoka SPD, chama cha Kansela, wanatetea sera ya maridhiano zaidi kwa Moscow.

Olaf Scholz, ambaye alimpokea mwenzake wa Ireland, ameelezea uamuzi wa Vladimir Putin kutambua uhuru wa maeneo yanayounga mkono Urusi mashariki mwa Ukraine kuwa ni shambulio dhidi ya sheria za kimataifa, kanuni za Umoja wa Mataifa na mikataba mingine iliyotiwa saini na Moscow kuhusu kuheshimu mipaka na uhuru wa mataifa.

Kansela wa Ujerumani amebaini kwamba kifurushi cha vikwazo vya Umoja wa Ulaya "kikubwa na chenye nguvu" dhidi ya Moscow kitawasilishwa siku ya Jumanne. Licha ya yote, mrithi wa Angela Merkel ametoa wito wa juhudi za kidiplomasia kati ya nchi za Magharibi na Urusi "kuepusha janga".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.