Pata taarifa kuu

Emmanuel Macron, Vladimir Putin na Volodymyr Zelensky wajadili mgogoro nchini Ukraine

Baada ya kuzungmza na rais wa Urusi, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameimpigia simu mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky kumjulisha kuhusu mazungumzo yao, Ikulu ya Élysée imetangaza Jumapili hii Februari 20, 2022.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, (kushoto, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (katikati), na Rais wa Urusi Vladimir Putin (kulia).
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, (kushoto, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (katikati), na Rais wa Urusi Vladimir Putin (kulia). Maksim BLINOV, Ludovic MARIN, Johanna GERON AFP
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo haya ya Emmanuel Macron, mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya na rais wa Urusi Vladimir Putin yameonekana katika masaa ya hivi karibuni kama yale yanayotoa nafasi ya mwisho ya kujadili kujiondoa kidiplomasia kwa mzozo wa Ukraine, huku ukiukaji wa usitishaji mapigano ukiongezeka.

“Mazungumzo ya simu na rais Putin yalidumu saa 1:45. rais wa jahmuri kwa sasa anazungumza kwa simu na rais Zelensky,” imesema ofisi ya rais wa Ufaransa.

Tayari Jumamosi jioni, kando ya mkutano wa usalama mjini Munich ambao wote wawili walishiriki, Emmanuel Macron alizungumza na mwenzake wa Ukraine ambaye alimwambia kwamba hataki "kujibu uchochezi kwenye maeneo hatari", kulingana na Ikulu ya Elysée.

Volodymyr Zelensky "alimwambia Vladimir Putin kuwa Ukraine iko tayari kwa mazungumzo", ofisi ya rais wa Ufaransa imebaini. "Hatua za kijeshi za Urusi dhidi ya Ukraine zitaleta vita katika katikati mwa Ulaya", kulingana na mshauri waa rais wa Ufaransa. Hakutakuwa na "chaguo lingine zaidi ya majibu yenye nguvu", ameongeza.

Putin na Zelensky wako tayari kujaribu kufikia usitishaji mapigano

Rais wa Urusi Vladimir Putin amehoji Jumapili hii mbele ya Emmanuel Macron "chokochoko" za Ukraine katika hali mbaya ya mapigano kati ya watu wanaotaka kujitenga mashariki mwa Ukraine, huku akisema anataka "kuongeza" juhudi za kidiplomasia kutatua mzozo huo.

Kulingana na Kremlin, Vladimir Putin pia ameomba, wakati wa mazungumzo haya ya simu na mwenzake wa Ufaransa, kwamba NATO na Marekani "zichukue kwa uzito" madai ya Urusi kuhusu usalama wake, kiini cha mzozo wa sasa kati ya Moscow na nchi za Magharibi. Marais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Vladimir Putin wa Urusi wamekubaliana Jumapili kufanya kila kitu ili kufikia haraka usitishaji mapigano mashariki mwa Ukraine, Ikulu ya Elysee imetangaza.

Rais wa Urusi Vladimir Putin alisisitiza kwa mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron "nia yake ya kuondoa wanajeshi wake" kutoka Belarus "mwishoni mwwa mazoezi ya sasa", imeongeza Ikulu ya Elysée.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.