Pata taarifa kuu

Ufaransa: Emmanuel Macron atangaza mpango mkubwa wa uzinduzi wa nyuklia

Wiki nane kabla ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa, Rais Emmanuel Macron amewasilisha Alhamisi hii, Februari 10, mkakati wake wa nishati kwa miaka thelathini ijayo. Kutoka Belfort, mashariki mwa nchi, rais wa Ufaransa ameamua kuweka nguvu za nyuklia zaidi ya hapo awali katika sera yake, njia pekee ya kuhakikisha uhuru wa nishati ya Ufaransa kulingana na Rais Emmanuel Macron.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akitoa hotuba mjini Belfort kuhusu ujenzi wa vinu vipya vya nyuklia nchini humo, Februari 10, 2022.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akitoa hotuba mjini Belfort kuhusu ujenzi wa vinu vipya vya nyuklia nchini humo, Februari 10, 2022. AP - Jean-Francois Badias
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza Alhamisi mpango mkubwa wa uzinduzi wa nyuklia, kwa lengo la ujenzi wa mitambo mipya sita ya kizazi cha pili kwa mwaka 2050, na kujadili ujenzi wa vinu vinane zaidi vya nyuklia.

Tangazo lingine, anataka "kupanua vinu vyote vinavyoweza kuongezwa", zaidi ya miaka 50 ikiwezekana.

"Nimefanya maamuzi mawili madhubuti: kupanua vinu vyote vya nyuklia ambavyo vinaweza kupanuliwa, bila kuacha chochote kile juu ya usalama" na "kwamba hakuna kinu cha nyuklia katika hali ya uzalishaji kitafungwa katika siku zijazo (...) isipokuwa kwa sababu za usalama. ", ametangaza Rais Emmanuel Macron huko Belfort, akibainisha kwamba alikuwa amemwomba idara inayohusika na masuala ya umeme EDF "kujadili masharti ya kuongeza muda wa zaidi ya miaka 50".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.