Pata taarifa kuu

Ukraine yadai silaha kutoka Ujerumani, Berlin yafutilia mbali hoja ya Kiev

Kutokana na mvutano wa sasa na vitisho vya uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, jumuiya ya kimataifa inahoji ikiwa ni muhimu kupeleka silaha kwa Kiev au la. Marekani imekuwa ikifanya hivyo kwa miaka kadhaa, nchi za Baltic, Uingereza, Jamhuri ya Czech wanataka kuchukua hatua hii ya Marekani. Berlin inakataa kufanya hivyo na imeitaka Estonia kutotuma silaha za Ujerumani kwa Ukraine.

Kansela Scholz wa Ujerumani amerudia kusema kuwa nchi yake haitapeleka silaha kwa Ukraine kwani Kiev imekuwa ikidai msaada wa kijeshi kutoka kwa Berlin kwa miaka mingi.
Kansela Scholz wa Ujerumani amerudia kusema kuwa nchi yake haitapeleka silaha kwa Ukraine kwani Kiev imekuwa ikidai msaada wa kijeshi kutoka kwa Berlin kwa miaka mingi. John MACDOUGALL POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mara nyingine siku Ijumaa, Januari 21, Kansela Scholz alirejelea kauli yake kwamba nchi yake haitapeleka silaha kwa Ukraine kwani Kiev imekuwa ikidai msaada wa kijeshi kutoka kwa Berlin kwa miaka mingi. Kwa upande wa Ujerumani, inasema diplomasia inasalia kuwa suluhisho bora zaidi kwa mzozo wa sasa. Uwasilishaji wa silaha kwa muungano mpya ungechochea tu mivutano iliyopo.

Berlin pia inataka kukaza sheria za sasa za uuzaji wa silaha usioidhinishwa kwa maeneo ambayo migogoro inafanyika. Hii inatumika pia kwa usafirishaji kupitia nchi za ulimwengu wa tatu. Ujerumani inakataa Estonia kupeleka silaha za Ujerumani huko Kiev.

Naye Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Christine Lambrecht katika mahojiano yaliyochapishwa na gazeti la Welt am Sonntag, amesema ingawa anatambua shauku ya Ukraine ya kupatiwa uungaji mkono mkubwa zaidi, lakini serikali ya Ujerumani haiko tayari kuipatia msaada wa silaha nchi hiyo na badala yake inawekeza nguvu katika kupunguza mvutano uliopo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.