Pata taarifa kuu

Papa Benedict XVI ahusishwa katika unyanyasaji wa watoto Ujerumani

Kanisa Katoliki la Ujerumani limetikiswa tena na kashfa ya unyanyasaji wa watoto. Ripoti ya unyanyasaji wa kijinsia uliofanywa tangu vita katika Jimbo kuu la Munich inatoa picha mbaya ya kushindwa kwa taasisi hiyo na kutilia shaka wajibu wa aliyekuwa kiongozi wa kanisa katoliki Benedict XVI.

Papa Benedict XVI akiwa Vatican, Februari 19, 2012.
Papa Benedict XVI akiwa Vatican, Februari 19, 2012. Reuters/Tony Gentile
Matangazo ya kibiashara

Majibu ya aliyekuwa Papa Benedict XVI kwa shutuma dhidi yake ni yanachukuwa kurasa 82. Mhusika anakanusha kuhusika na kesi nne za unyanyasaji wa kijinsia ambazo inadaiwa alificha alipokuwa Askofu Mkuu wa Munich kati ya mwaka 1977 na 1982.

Waandishi wa ripoti hiyo wanafikia hitimisho tofauti. Wanaamini kwamba Kadinali Joseph Ratzinger hakuchukua hatua yoyote ya kuwaondoa makasisi wanne wenye hatia ya kuwabaka watoto wadogo wakati papa huyo wa zamani alijua mielekeo na malezi yao. Kesi ya kasisi Peter Hullermann inachukuwa si chini ya kurasa 370 kati ya 1,700 katika ripoti hiyo.

Ripoti hiyo, ilioagizwa na askofu mkuu wa Munich, inakadiria kuwa watoto 500 walikuwa waathiriwa wa vitendo kama hivyo tangu vita na inazungumzia juu ya "rekodi mbaya". Warithi wawili wa aliyekuwa kiongozi wa kanisa Katoliki pia wamehusishwa na kashfa hiyo.

Kanisa Katoliki la Ujerumani limekuwa likitikiswa na ufichuzi kuhusu makasisi wanaolawiti watoto kwa zaidi ya miaka kumi. Theluthi mbili ya dayosisi imezindua tafiti, mara nyingi chini ya shinikizo kutoka nje. Waathiriwa wanakosoa fidia isiyotosha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.