Pata taarifa kuu
ULAYA-JAMII

EU yataka kulinda haki za kijamii za wafanyakazi kwenye kampuni kama vile Uber au Deliveroo

Umoja wa Ulaya unabaini kwamba kampuni 500 au zaidi zinzofanya kazi barani Ulaya lazima ziheshimu haki za kijamii za wafanyakazi wao ambao tayari wametekeleza zaidi ya kesi mia moja dhidi yao katika Umoja huo.

Kwa upande wa Nicolas Schmitt, Kamishna anayehusika na ajira na masuala ya kijamii, anasema neno la msingi sasa litakuwa dhana ya mshahara. Wafanyakazi wa kampuni watachukuliwa kuwa wafanyakazi walioajiriwa chini ya mkataba.
Kwa upande wa Nicolas Schmitt, Kamishna anayehusika na ajira na masuala ya kijamii, anasema neno la msingi sasa litakuwa dhana ya mshahara. Wafanyakazi wa kampuni watachukuliwa kuwa wafanyakazi walioajiriwa chini ya mkataba. AFP
Matangazo ya kibiashara

Tume ya Ulaya inataka kuunga mkono uchumi mpya na hasa tasnia ya kampuni kama Uber au Deliveroo kwa mfano, ambazo inawakilisha mauzo ya kila mwaka ya euro bilioni ishirini katika umoja huo na ambayo kulingana nayo itaajiri raia wa Ulaya milioni 43 ndani ya miaka minne. Lakini kulingana na taasisi hiyo, maendeleo haya lazima yafanyike "Ulaya" na haki za kijamii zilizojengwa kwa zaidi ya karne katika bara hili la zamani.

Kati ya raia wa Ulaya milioni 28 wanaofanya kazi kwenye kampuni kama vile watu wanaosafirisha mizigo au madereva, kwa mfano, zaidi ya milioni tano na nusu hawana hadhi ifaayo. Katika idadi kubwa ya kesi hawakujichagua wenyewe na kujikuta wakichukuliwa kama wafanyakazi wanaojitegemea.

Dhana ya kutolipwa mishahara

Kwa upande wa Nicolas Schmitt, Kamishna anayehusika na ajira na masuala ya kijamii, anasema neno la msingi sasa litakuwa dhana ya mshahara. Wafanyakazi wa majukwaa watachukuliwa kuwa wafanyakazi walioajiriwa chini ya mkataba.

"Kuanzia wakati mtu anafanya kazi kama mwajiriwa, kama mfanyakazi, tumeanzisha idadi fulani ya vigezo ... lazima achukuliwe kama mwajiriwa na apewe haki za wafanyakazi," anasema. Sheria zetu zote za kazi zinatokana na wazo hili la utii. Wakati mwajiri wako anakudhibiti, anaporekebisha malipo yako au wakati kuna ufuatiliaji wa wakati wako wa kufanya kazi, wewe ni mwajiriwa, wewe sio mfanyakazi anayejitegemea ".

Tume ya Ulaya imeweka vigezo vitano kama vile kuweka kupitia jukwaa la sheria juu ya njia ya kufanya kazi au malipo, usimamizi au jinsi ya kufanya kazi. Inakadiria kuwa kati ya wafanyakazi milioni mbili hadi nne wa kampuni wanaweza kuchukuliwa kama wafanyakazi kutokana na pendekezo lake na hivyo kunufaika na likizo ya kulipwa, haki za pensheni, ulinzi wa kijamii au mshahara wa chini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.