Pata taarifa kuu

Bulgaria: Watu kadhaa wafariki dunia katika ajali ya basi kusini mwa Sofia

Takriban watu 45 wamefariki dunia usiku wa Jumatatu 22 kuamkia Jumanne Novemba 23 nchini Bulgaria katika ajali ya basi lililokuwa na raia wa Macedonia Kaskazini. Ni abiria saba tu ndio waleweza kuokolewa.

Basi hilo lilianguka eneo baya kwenye barabara kuu kati ya Bulgaria na Ugiriki.
Basi hilo lilianguka eneo baya kwenye barabara kuu kati ya Bulgaria na Ugiriki. © DIMITAR KYOSEMARLIEV / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Watu arobaini na tano au arobaini na sita walifariki dunia" katika mkasa huu ambao uliotokea karibu na ane usiku (saa za Bulgaria) kwenye barabara kuu karibu na kijiji cha Bosnek, kilomita 40 kusini mwa Sofia, amesema Kamishna Nikolay Nikolov, mkuu wa idara inayokabiliana na majanga kwenye televisheni ya umma ya BNT. "Abiria saba waliokolewa" na kupelekwa hadi hospitalini katika mji mkuu, ameongeza. "Dereva alifariki papo hapo, kwa hivyo hakukuwa na mtu wa kufungua milango" na kuwezesha abiria kuepuka moto, Mkuu wa Polisi nchini Bulgaria Stanimir Stanev amesema kwenye kituo kingine cha habari.

Basi hilo lilianguka eneo baya kwenye barabara kuu kati ya Bulgaria na Ugiriki. Bado haijabainika iwapo ilishika moto kabla au baada ya ajali hiyo. Watu saba walionusurika, waliopelekwa kwenye chumba cha dharura huko Sofia, wako katika hali mbaya lakini wanaendelea vizuri. Katika ushuhuda wao, wanazungumzia "mlipuko mkubwa" ambao uliwaamsha abiria waliokuwa wamelala, anaripoti mwandishi wetu wa Sofia, Damian Vodénitcharov. Walionusurika walilazimika kuvunja madirisha ili kujiokoa. Sababu za ajali hiyo bado hazijajulikana na kwa maoni ya wataalamu, itachukua miezi kadhaa kwa uchunguzi kubaini sababu hizo.

Barabara hiyo ilikuwa imekarabatiwa hivi majuzi kwa fedha za Umoja wa Ulaya, ambapo Bulgaria imekuwa mwanachama wake tangu 2007. Kulingana na kituo cha bTV, watoto kumi na wawili walikuwa kwenye gari hilo, ambalo lilitoka Istanbul na lilikuwa likielekea Skopje. "Ni msiba. Hatujui ikiwa waathiriwa wote wanatoka Makedonia Kaskazini, lakini ndivyo tunavyofikiria kwa sababu basi hilo limesajiliwa nchini humo", amejibu kwa upande wake Waziri Mkuu wa Macedonia Kaskazini Zoran Zaev, akihojiwa na televisheni ya Nova.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.