Pata taarifa kuu
UFARANSA-HAKI

Macron na Badinter waomba "kufutwa kwa adhabu ya kifo duniani wote"

Rais wa Ufaransa ameongoza maadhimisho ya miaka 40 tangu nchi hiyo ilipozuia adhabu ya kifo, huku akito wito kwa adhabu hiyo kufutwa kote duniani.

© Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Macron ameelezea adhabu ya kifo kama kitendo kisichostahili na kuahidi kuandaa mkutano mwaka ujao, kushinikiza adhabu hiyo kuondolewa duniani.

Sherehe iliandaliwa asubuhi katika Panthéon, eneo la jamhuri ambapo vongozi wakuu katika historia ya Ufaransa walizikwa, na hasa watetezi dhidi ya adhabu ya kifo, kama vile Victor Hugo na Jean Jaurès mbele ya rais Macron na Robert Badinter, 93, waziri wa zamani sheria  katika utawala wa François Mitterrand na mtetezi wa kufutwa adhabu hiyo.

"Hukumu ya kifo inatakiwa kutoweka ulimwenguni kwa sababu ni aibu kwa ubinadamu", amesema waziri wa zamani wa sheria na wakili. "Haki ya Ufaransa haitakuwa tena haki ya kuuaa", amebaini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.