Pata taarifa kuu

Umoja wa Ulaya wakabiliwa na ongezeko la bei ya nishati

Uhispania, Ugiriki, Romania, Jamhuri ya Czech na Ufaransa wamewataka washrika wao wa Ulaya kutoa wito wa kuchukua hatua kwa pamoja kuhusiana na bei ya nishati.

Kuongezeka kwa gharama za nishati: Tume ya Ulaya inandaa "mikakati ya kukabiliana na suala hilo".
Kuongezeka kwa gharama za nishati: Tume ya Ulaya inandaa "mikakati ya kukabiliana na suala hilo". AFP PHOTO / BORIS HORVAT
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri wa mazingira wanajadili suala hili Jumatano na viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya watalijadilia kwa njia rasmi katika mkutano wa viongozi wa Ulaya uliopangwa kufanyika Oktoba 21 hadi 22.

Tume ya Ulaya inandaa kukabiliana na kupanda kwa bei ya nishati, vyombo na msaada ili kusaidia wanunuzi, lakini mikakati hii inalenga kuruhusu misaada ya kitaifa iliyo katika maandalizi au tayari inatumika. Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen, ametaja wazo la kutenga hifadhi ya kimkakati, akiunga mkono pendekezo la Uhispania la kutumia manunuzi ya pamoja kupitia nchi za Umoja wa Ulaya zilizostawi kiuchumi ili kupata bei ya nafuu.

Kwa upande mwingine bei ya mafuta ya petroli barani Afrika inatazamiwa kupanda katika wiki za hivi karibuni kutokana na matokeo yaliyosababishwa na kuongezeka ama kupanda kwa bei ya mafuta duniani, kwa mujibu wa wachambuzi.

Kupanda kwa bei ya mafuta duniani inaweza kuongeza mapato kwa muda mfupi , lakini thamani halisi itaonekana wakati wazalishaji wa mafuta watakavyoweza kuzalisha na kukidhi mahitaji ya usambazaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.