Pata taarifa kuu

Catalonia: Carles Puigdemont arejea Brussels

Baada ya kushutumiwa na mahakama ya Uhispania kwa jukumu lake katika jaribio la kujitenga kwa jimbo la Catalonia mnamo 2017, kiongozi wa zamani wa jimbo hilo Carles Puigdemont alikamatwa nchini Italia.

Carles Puigdemont asiste a la Comisión de Comercio Internacional del Parlamento Europeo en Bruselas, el 27 de septiembre de 2021
Carles Puigdemont asiste a la Comisión de Comercio Internacional del Parlamento Europeo en Bruselas, el 27 de septiembre de 2021 François WALSCHAERTS AFP
Matangazo ya kibiashara

Carles Puigdemont, ambaye alishtakiwa nchini Uhispania kwa jukumu lake katika jaribio la kujitenga kwa jimbo la Catalonia mnamo mwaka 2017, amewasili mjini Brussels nchini Ubelgiji Jumatatu wiki hii baada ya kukamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Italia, wakili wake Gonzalo Boye ameliambia shirika la habarila AFP.

"Yuko Brussels na atarudi Sardinia Jumapili" kuhudhuria kikao cha Mahakama Jumatatu ijayo kuhusu kupelekwa kwake nchini Uhispania, wakili huyo amesema katika ujumbe.

Carles Puigdemont, 58, ambaye kwa sasa anaishi nchini Ubelgiji, ambako alikimbilia mnamo 2017 akikwepa mashtaka ya mahakama ya Uhispania, alikamatwa Alhamisi jioni wiki iliyopita alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Alghero, kisiwa cha Italia, ambapo angeshiriki  tamasha la Adifolk. Aliachiliwa Ijumaa jioni baada ya kuahidi kurudi Sardinia kusikiliza kesi inayomhusu ya kupelekwa nchini Uhespania.

Mahakama ya Uhispania inamshutumu Carles Puigdemont kwa "uchochezi" na "ubadhirifu wa pesa za umma" kwa jukumu lake katika jaribio la kujitenga la 2017, moja ya mzozo mbaya zaidi uliyoikumba Uhispania tangu kumalizika kwa udikteta wa Franco mnamo 1975.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.