Pata taarifa kuu
EU

Idadi ya raia wa Syira na Afghanistan wanaoingia EU kupitia Balkan yaongezeka

Idadi ya wahamiaji haramu wanaoingia katika nchi za Umoja wa Ulaya kwa kupitia Balkan imeongezeka mara mbili mwaka huu, shirika linalojihusisha na ulinzi wa mipaka ya nje ya EU, Frontex, limesema Alhamisi wiki hii, na kuongeza kuwa wengi wao ni raia wa Syria na Afghanistan.

Frontex, shirika linalojihusisha na ulinzi wa mipaka ya nje ya EU, linathibitisha kwamba idadi ya wakimbizi wanaoingia Ulaya imongezeka.
Frontex, shirika linalojihusisha na ulinzi wa mipaka ya nje ya EU, linathibitisha kwamba idadi ya wakimbizi wanaoingia Ulaya imongezeka. REUTERS/Darrin Zammit
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na shirika la Frontex, wahamiaji 22,600 waligunduliwa wakati waliingia kinyume cha sheria katika nchi za Umoja wa Ulaya kupitia Balkan za Magharibi kati ya mwezi Januari na Julai, ongezeko la 90% ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Shirika hilo limesema katika taarifa kwamba mnamo mwezi Julai pekee, idadi ya wahamiaji haramu wanaotumia njia hiyo iliongezeka kwa 67%.

Nchi nyingi wanachama wa Umoja wa Ulaya zinafuata kwa wasiwasi mkubwa hali inayoendelea nchini Afghanistan, ambapo waasi wa Taliban wanazidisha mashambulizi nchini kote na wamepata mafanikio makubwa katika siku za hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.