Pata taarifa kuu
UJERUMANI-USALAMA

Raia wa Uingereza akamatwa Ujerumani kwa madai ya upeleleza kwa niaba ya Urusi

Polisi ya Ujerumani Jumanne imemkamata raia wa Uingereza anayefanya kazi katika ubalozi wa Uingereza huko Berlin kwa madai ya kupeleka nyaraka kwa idara  ya ujasusi ya Urusi, vyombo vy sheria vya Ujerumani vimebaini Jumatano.

"Mtuhumiwa alipokea pesa kwa kiasi ambacho bado hakijulikani baada ya kupeleka habari hiyo," imesema taarifa hiyo.
"Mtuhumiwa alipokea pesa kwa kiasi ambacho bado hakijulikani baada ya kupeleka habari hiyo," imesema taarifa hiyo. © laMinuteInfo
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na ofisi ya mashtaka ya shirikisho, upekuzi ulifanywa mahali pa kazi na nyumbani kwa mtuhumiwa, aliyejulikana kama David S. Ametakiwa kufika mbele ya jaji wa ucunguzi baadaye Jumatano.

"Angalau mara moja, aliwasilisha hati ambazo alikuwa amepata wakati wa shughuli zake za kazi kwa mwakilishi wa idara ya ujasusi ya Urusi," ofisi ya mwendesha mashtaka wa shirikisho ilisema katika taarifa.

"Mtuhumiwa alipokea pesa kwa kiasi ambacho bado hakijulikani baada ya kupeleka habari hiyo," imesema taarifa hiyo.

Mtu huyo alikamatwa Jumanne karibu na mji wa Berlin huko Potsdam, mji mkuu wa jimbo la Brandenburg. Polisi ya Ujerumani imesema mshukiwa alikuwa mfanyakazi wa ubalozi wa eneo hilo hadi alipokamatwa. Polisi wa Uingereza inasema ana miaka 57.

Kukamatwa kwake ni matokeo ya uchunguzi uliofanywa kwa pamoja na mamlaka ya Ujerumani na Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.