Pata taarifa kuu
CYPRUS

Cyprus: UNSC yalaani mpango wa kufungua tena Varosha

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshtumu katika taarifa Ijumaa hatua ya Uturuki na Cyprus ya Uturuki kufunuliwa kwa upande mmoja wa sehemu ya Varosha na kutaka kufutwa kwa hatua hii mara moja.

Watalii kwenye pwani karibu na pwani iliyowekewa uzio katika mji wa Varosha, unaodhibitiwa na jeshi la Uturuki, kaskazini mwa Cyprus.
Watalii kwenye pwani karibu na pwani iliyowekewa uzio katika mji wa Varosha, unaodhibitiwa na jeshi la Uturuki, kaskazini mwa Cyprus. AFP
Matangazo ya kibiashara

"Baraza la Usalama linasisitiza umuhimu wa kuzuia hatua yoyote ya upande mmoja ambayo inakwenda kinyume na maazimio yake na ambayo inaweza kuongeza mvutano katika kisiwa (cha Cyprus) na kudhoofisha matarajio ya suluhu," wajumbe Kumi na Tano wa baraza hilo wamesema.

Katika ziara yake siku ya Jumanne katika mji mkuu uliogawanyika wa kisiwa cha Mediterranean, kuadhimisha udhibiti wa sehemu ya kaskazini ya Cyprus na jeshi la Uturuki Julai 20, 1974, rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alitangaza kuendelea na zoezi la kufunguliwa kwa mji wa Varosha (Maras kwa Kituruki), eneo la kale la mapumziko ambalo kutelekezwa kwake kunaashiria mgawanyiko wa kisiwa hicho.

Cyprus imegawanyika tangu  mwaka1974 kati ya sehemu ya Uigiriki inayotambuliwa na Umoja wa Ulaya na sehemu ya Uturuki isiyotambuliwa na jamii ya kimataifa, isipokuwa Ankara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.