Pata taarifa kuu
UFARANSA - AFYA

Ufaransa kushuhudia wimbi la nne la maambukizi ya Covid -19

Mshauri wa serikali ya Ufaransa kuhusu mwenendo wa virusi wa vya corona, Profesa Jean-François Delfraissy, amesema huenda taifa hilo likashuhudia wimbi la nne la maambukizi ya Covid 19, kutokana na idadi ya juu ya maambukizi inayotokana na virusi aina ya Delta, vilivyotambulika nchini India.

Waziri wa afya nchini Ufaransa, Olivier Véran
Waziri wa afya nchini Ufaransa, Olivier Véran AP - Thomas Samson
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Delfraissy, ameongeza kuwa kutolewa kwa kasi kwa chanjo ya Covid-19, kunaweza saidia kupunguza idadi ya maambukizi ya virusi vya corona, na kuzuia wimbi la nne linalotarajiwa mwezi Septemba au Oktoba.

Waziri wa afya nchini humo, Olivier Veran, mapema juma hili amesema virusi aina ya Delta, ambayo vimechangia baadhi ya mataifa kutangaza marufuku ya usafiri, vinawakilisha asilimia 20 ya maambukizi ya Covid 19 nchini Ufaransa.

Kufikia sasa Ufaransa imesajili visa millioni 182 vya maambukizi ya corona pamoja na vifo millioni 3.9.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.