Pata taarifa kuu
IRAN-HAKI

Benjamin Brière anayeshikiliwa Iran akabiliwa na mashitaka ya ujasusi

Mfaransa huyo, ambaye aliingia nchini Iran kama mtalii, atahukumiwa kwa "ujasusi" na "propaganda" dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, kulingana na wakili wake. Benjamin Brière anazuiliwa jela nchini Iran tangu mwezi Mei 2020.

Picha ya Benjamin Brière aliyekamatwa mwezi Mei 2020 anatuhumiwa kupiga picha katika maeneo ya jeshi.
Picha ya Benjamin Brière aliyekamatwa mwezi Mei 2020 anatuhumiwa kupiga picha katika maeneo ya jeshi. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Raia huyo wa Ufaransa, aliyezuiliwa nchini Iran kwa mwaka mmoja, anashikiliwa katika gereza la Vakilabad, katika mji mtakatifu wa Mashhad, ulioko kaskazini mashariki mwa Iran.

Benjamin Brière atahukumiwa kwa "ujasusi" na "propaganda dhidi ya serikali" na mahakama ya mapinduzi ya nchi hiyo, wakili wake ametangaza Jumapili hii, Mei 30. Hakuna maelezo yaliyotolewa juu ya tarehe ya kesi na mashtaka. Lakini kulingana na vyombo vya habari nchini Iran, anatuhumiwa hasa kwa piga picha na kunasa video za maeneo ya jeshi.

Alikuwa akisafiri nchini Iran katika gari lake. Alikamatwa mbali na mji wa Mashhad. Kando ya barabara kati ya Tehran na jiji hili, kuna kambi kadhaa muhimu za jeshi, hususan maeneo ya kurushia makombora ya masafa marefu.

Benjamin Brière, 30, pia anatuhumiwa kudharau kivazi cha niqab kwenye jumbe zake katika mitandao ya kijamii.

Kubadilishana wafungwa

Kesi hiyo inakuja wakati Iran inamshikilia mtafiti kutoka Ufaransa mwenye asili ya Iran Fariba Adelkhah, aliyehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kitendo cha kuhatarisha usalama wa taifa na propaganda dhidi ya serikali.

Katika miaka ya hivi karibuni, Iran ilibadilishana wafungwa kadhaa wa kigeni au wale wenye uraia pacha na raia wa Iran waliokuwa kizuizini nchini Ufaransa, Australia na Marekani.

Walakini, mwanzoni mwa mwezi Mei, mwanadiplomasia wa Iran, Assadollah Assadi, alihukumiwa Ubelgiji kifungo cha miaka 20 gerezani kama sehemu ya uchunguzi wa shambulio lililopangwa karibu na mji wa Paris likiwalenga wapinzani wa Iran.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.