Pata taarifa kuu
ITALIA

Mario Draghi kutawazwa kuongoza Italia

Mario Draghi anatarajiwa kuapishwa leo Jumamosi baada ya kupata idadi kubwa ya wabunge siku moja kabla, na kutangaza serikali yake, kwa lengo la kuiondoa Italia katika mizozo ya kisiasa na kiafya.

Mario Draghi, waziri mkuu mpya wa Italia.
Mario Draghi, waziri mkuu mpya wa Italia. REUTERS/Ints Kalnins
Matangazo ya kibiashara

Bwana Draghi, kwa jina maarufu "Super Mario" kutokana na jukumu lake katika mgogoro wa deni la ukanda wa euro mnamo mwaka 2012, atasimama mbele ya Bunge la Seneti Jumatano wiuki ijayo na kisha mbele ya Baraza la Wawakilishi Alhamisi kwa kura ya kuwa na imani naye, hatua ambayo itatoa uhalali wa mwisho kwa serikali yake.

Rais wa zamani wa Benki Kuu ya Ulaya (ECB), aliyechaguliwa na rais wa Jamhuri Sergio Mattarella kumrithi Giuseppe Conte, aliyelazimishwa kujiuzulu baada ya muungano wake kuvunjika, alimteua mtu wa anayemuamini, Daniele Franco, kushikilia Wizara muhimu ya Uchumi.

Draghi mwenye umri wa miaka 73, alijitokeza mbele ya vyombo vya habari baada ya tangazo lililotolewa na msemaji wa kasri la rais, na kutangaza baraza lake la mawaziri, linaloundwa na wanasiasa na watalaamu.

Awali, Draghi alifanya mashauriano mapana na wawakilishi wa vyama mjini Rome, na alipata uungwaji mkono wa kushangaza kutoka muungano wa shoto ulioshindwa wa mtangulizi wake Giuseppe Conte, pamoja na upinzani.

Mzozo wa serikali nchini Italia, katikati mwa janga la virusi vya Corona, umeendelea tangu katikati mwa mwezi Januari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.